ITIKADI YA MASHIA[4] Surat Al-Hashr Aya ya 23-24

[5] Surat Az-Zukhruf Aya ya 84

[6] Surat Al-Hadiyd Aya ya 4

[7] Surat Qaf Aya ya 16

[8] Surat Al-Hadiyd Aya ya 3.

[9] Suratul-Buruj Aya ya 15

[10] Surat     , Baadhi ya Aya za qur-ani, zinathibitisha kuwa, kiti cha ufalme wa Mwenyeezi Mungu kimeenea mbinguni na ardhini, kwa hiyo, ufalme na mamlaka ya Mwenyeezi Mungu yameenea ulimwengu mzima, kama tunayosoma  katika Suratul-Baqarah Aya ya 255.

اللّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَاْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِى السَّمَاوَاتِ وَمَا فِى الاَرْضِ مَن ذَا الَّذِى يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ اَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu

Maelezo kuhusiana na Aya ya 255 ya Suratul-Baqarah

Aya hii huitwa Ayatul-Kursiyyu, aya tukufu kabisa, anahimizwa kila Muislamu kuyaweka maana ya Aya hii mbele ya macho yke daima, ili asimuone muqaddim wala muakhkhir, ila Mwenyewe tu Mwenyeezi Mungu Subhanahu Wataala, na mahala pengi katika hadithi za Mtume amehimizwa mtu kuisoma, kama

a) Baada ya kutoa salamu katika sala, b) kabla ya kulala, c) anapotoka nje, d) anapoingia ndani,

e) anapokuwa na hofu ya kuogopa vinavyoonekana na visivyoonekana.

[11] Surat Ash-Shuura Aya ya 11

[12] Surat At-Tawhiyd Aya ya 4back 1 2 3 4 5 6 7 8 9