ITIKADI YA MASHIAAya hiyo haina maana ya kuwa; Mwenyeezi Mungu ana sehemu au zama maalumu, bali inathibitisha utukufu wa utawala wake katika ulimwengu mzima wa kimada na ule usiokuwa wa kimada, kwa sababu kama tukijaalia kuwa Mwenyeezi Mungu sehemu au zama maalumu, tutakuwa tumemuweka Mwenyeezi Mungu katika mipaka maalumu, na tumempa sifa ya viumbe, na tutakuwa tumemfahamu Mwenyeezi Mungu kama tunavyovifahamu vitu vyengine vya kikawaida hali ya kwamba Yeye Mwenyewe Mola Mtakatifu anasema:-

فَاطِرُ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ جَعَلَ لَكُم مِّنْ اَنفُسِكُمْ اَزْوَاجاً وَمِنَ الاَنْعَامِ اَزْوَاجاً يَذْرَؤُكُمْ فِيهِ لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ[11]

Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika nyama hoa dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.

Na katika Aya nyengine anasema:-

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُواً اَحَدٌ[12]

Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.

Hizo zilikuwa ni miongoni mwa itikadi za Shia Ithna Asharia, tutaendelea kuelezea itikadi nyengine katika makala zinazofuata.[1] Surat Al-Imrani Aya ya 193

[2] Surat Adh-Dhariyat Aya ya 20-21

[3] Surat al-Imrani Aya ya 190-191back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 next