ITIKADI YA MASHIAMaelezo yanayopatikana katika Aya hiyo.

Aya hiyo inataja ujuzi wa Mwenyeezi Mungu na uweza wake.

هُوَ الاَوَّلُ وَالآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ[8]

Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhaahiri na wa Siri, naye ndiye Mjuzi wa kila kitu.

Kwa hiyo, ikiwa katika Qur-ani tunasoma:-

ذُو الْعَرْشِ الْمَجِيدُ[9]

Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu,

Neno “ARSHI” lililokuja katika Aya hiyo halimaanishi kiti cha ufalme, bali linamaanisha utukufu na mamlaka yake Allah (s.w), na ikiwa katika Qur-ani tunasoma:

[10] اللهُ الَّذِى خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِى سِتَّةِ اَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَي عَلـٰي الْعَرْشِ مَا لَكُم مِّن دُونِهِ مِن وَلِيٍّ وَلاَ شَفِيعٍ اَفَلاَ تَتَذَكَّرُونَ

Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki?back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 next