ITIKADI YA MASHIA3. DHATI YA ALLAH (S.W) IMETAKASIKANA ISIYOKUWA NA MWISHO.

Sisi tunaamini kuwa dhati  ya Mwenyeezi Mungu imeenea sehemu zote, naye hana mwanzo wala mwisho, dhati hiyo inaonekana katika elimu yake, qudra ya utukufu wake, kubakia kwake milele katika sehemu zote na zama zote, na kwa sababu hiyo basi ndio tukasema kuwa Mwenyeezi Mungu hana sehemu maalumu wala kipindi maalumu, kwa sababu sehemu au nafasi na zama zina kiwango maalumu, ijapokuwa Mwenyeezi Mungu hana sehemu maalumu wala zama maalumu lakini Yeye yuko katika sehemu na zama zote, kwa sababu dhati ya utukufu wake ni iko juu zaidi kuliko sehemu na zama, kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-

وَهُوَ الَّذِى فِى السَّمَاء إِلَهٌ وَفِى الاَرْضِ إِلَهٌ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ[5]

Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hikima, Mwenye ujuzi.

هُوَ الَّذِى خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضَ فِى سِتَّةِ اَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَي عَلـٰي الْعَرْشِ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِى الاَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاء وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا وَهُوَ مَعَكُمْ اَيْنَ مَا كُنتُمْ وَاللهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ[6]

 

Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha akakaa vyema juu ya enzi. Anayajua yanayo ingia katika ardhi na yanayo toka humo, na yanayo teremka kutoka mbinguni, na yanayo panda humo. Naye yu pamoja nanyi popote mlipo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayo yatenda.

Ndio, Mwenyeezi Mungu yuko karibu na wanaadamu, na Mwenyeezi Mungu yuko ndani ya nafsi za wanaadamu, Naye yuko katika sehemu zote, hali ya kwamba hana sehemu, makani, wala zama maalumu.

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ وَنَحْنُ اَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ[7]

Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 next