ITIKADI YA MASHIAHakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili.

Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto.

2. SIFA TUKUFU ZA KIJALALI NA KIJAMALA ZA ALLAH (S.W).

Sisi tuna itikadi ya kuwa; Mwenyeezi Mungu (s.w) ametakasika na kila aibu, Mwenyeezi Mungu ni mkamilifu wa kila kitu, kwa maelezo mengine, kila jema, na kila kamilifu liliopo katika ulimwengu huu linatokana na dhati iliyotakasika yake Yeye Allah (s.w).

هُوَ اللهُ الَّذِى لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلاَمُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ سُبْحَانَ اللهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ. هُوَ اللهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ لَهُ الاَسْمَاء الْحُسْنَي يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِى السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ[4]

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hekima.

Maelezo kuhusiana na Aya:

Aya hizo zinataja sifa nyingi za Mwenyeezi Mungu, sifa ambazo zimeelezewa fadhila zake katika hadithi nyingi za Mtume Muhammad

 (s.a. w.w). katika sehemu hii tutaelezea sifa za kijalali na kijamala za Mola Mtakatifu.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 next