ITIKADI YA MASHIANjia bora inayoweza kuyafanya madhehebu kufahamiana ni kutambuana kupitia misingi ya dini yao ya Kiislamu, na kutambuana akida zao kupitia maulamaa wao maarufu waliobobea kielimu na wanaotambulika katika jamii, kwa sababu ikiwa watafahamiana akida zao kupitia wafuasi wa madhehebu yao, wafuasi ambao hawana elimu ya kutosha inayohusiana na akida zao, na wafuasi wa madhehebu tofauti wakajenga uadui na kuekeana chuki kutokana na ikhitilafu walizonazo, hapana shaka uadui na chuki hizo itafunga na kuzuia njia zitakazowapeleka katika mashirikiano, na mafahamiano au mashirikiano yatabadilika na kuwafanya waislamu hao watengane kutokana na tofauti zao za kiakida na kiamali.

3. Kwa mujibu wa vidokezo viwili hivyo, tulivyovielezea hapo juu, ndio tukaamua kuelezea misingi ya akida za Kiislamu zinazoendana sambamba na sifa au akida za madhehebu ya Shia, katika kitabu hiki tutaelezea kwa ufupi sifa za kitabu hiki.

1. kitabu hiki kimekusanya maudhui yote yanayohusiana na itikadi za madhehebu ya Shia, maudhui ambayo yameelezewa kwa ufupi, hii itawaondolea tabu itakayoweza kuwapata wasomaji wa kitabu hiki kutotalii vitabu tofauti, (kwani kitabu hiki kimekusanya maudhui yote, hivyo kwa kutalii kitabu hiki tu wanaweza kupata kila wanalohitajia kulielewa).

2. Maelezo ya kitabu hiki yameelezewa kwa uwazi kabisa bila ya kuonekana utata wowote, na wala hakukutumiwa istilaha ambazo hutumika katika mazingira ya kielimu au madrasa za kidini tu, na kutofanya hivyo hakukuleta upungufu wowote katika mabainisho ya maudhi hayo.

3. Ijapokuwa malengo ni kubainisha akida za madhehebu ya Shia, na sio kubainisha dalili zake, lakini baadhi ya maudhui yameelezewa kupitia dalili za Qur-ani, sunna, na dalili za kiakili.

4. Maelezo ya kitabu hiki yameelezewa kwa uwazi kabisa, ili kuonyesha uhakika wa itikadi zao ulivyo.

5. Katika uandishi wa kitabu hiki kumezingatiwa adabu na desturi za madhehebu yote na katika maudhui yote.

Kitabu hicho, kimetayarishwa muandishi huyo, wakati alipokuwa katika safari yake ya hija ya kuzuru nyumba takatifu ya Mwenyeezi Mungu (Baytulahil-haram), na kimepitishwa na kukubaliwa na vitengo vya dini baada ya kuwekwa vikao mbali mbali, vikao ambavyo maulamaa walijadiliana na kutoa nadharia zao kuhusiana na maudhui yaliyoandikwa katika kitabu hicho, hivyo tuna matumaini ya kuwa tutafikia yale malengo yaliyokusudiwa ya kuandikwa kitabu hiki, malengo ambayo tuliyaashiria hapo mwanzo, na kuwa uthibitisho na ithbati ya siku ya Kiama, hivyo tunamuelekea Mola wetu na kumuomba kwa kusema:-

رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِياً يُنَادِى لِلإِيمَانِ اَنْ آمِنُواْ بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الابْرَارِ[1]

  Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi; nasi tukaamini. Basi tusamehe madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na utufishe pamoja na watu wema.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 next