ITIKADI YA MASHIA
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

ITIKADI YA SHIA ITHNA ASHARIA

MALENGO YA KUBAINISHWA UJUMBE WA ITIKADI YA SHIA ITHNA ASHARIA.

1. Watu wote ulimwenguni, katika zama hizi wanashuhudia mabadiliko makubwa. mabadiliko ambayo yanatokana na dini kubwa miongoni mwa dini tukufu za Mwenyeezi Mungu (s.w), nayo ni dini ya Kiislamu.

Katika zama za leo, Uislamu umehuwika na kukua tena, na Waislamu wote duniani wameamka na kuzinduka katika butwaa waliyokuwa nayo, na wamerudia katika yale mambo ya thamani yanayowapa na kuonyesha hadhi yao ulimwenguni, Waislamu wanapotaka kutatua matatzo yao, au kuyatafutia ufumbuzi hawarejei kitu chengine isipokuwa hutafuta au kurejea katika taaluma na misingi yao ya dini ya Kiislamu.

Ni dalili gani basi iliyoleta mabadiliko hayo? maudhui hayo tutayaelezea kwa upande wake, jambo muhimu linalotupasa kulielewa ni kuwa; athari nzuri zilizopatikana kutokana na mabadiliko hayo zimeenea katika nchi zote za kiislamu, na zimedhihirika hata katika nchi zisizokuwa za Kiislamu, na ni kwa sababu hiyo basi, watu wengi duniani wanataka kutambua dini ya Kiislamu inasema nini? au ina maelezo gani? na imeleta ujumbe gani mpya kwa watu wote duniani?.

Katika hali kama hiyo basi, ni wadhifa wetu sisi Waislamu, kuiarifisha na kuisambaza dini ya Kiislamu na Uislamu vile ulivyo. kiasi ya kwamba uarifishaji na uelezeaji huo utapelekea watu kuifahamu dini hiyo takatifu, ili wale wenye kiu na wanaohitaji kuielewa dini ya Kiislamu waweze kuielewa na kupata taaluma zaidi inayohusiana na dini hiyo, na wala tusiwakubalie watu wengine (wasiokuwa Waislamu) kuiarifisha dini hiyo na kutoa maamuzi yao yasiyoendana sambamba na dini hiyo au itikadi zetu.

2. Ni jambo lililo wazi na lisilopingika kuwa; dini ya Kiislamu mfano wa dini nyengine ina madhehebu tofauti, na kila dhehebu lina sifa zake katika mambo ya akida na namna ya utendaji wa amali kutokana na akida hizo wanazoziamini, lakini tofauti hizo sio kubwa kiasi ambacho pasiwe na uwezekano wa kutoshirikiana baina ya wafuasi wa dhehebu fulani na wafuasi wa dhehebu jengine, bali wafuasi hao wa madhehebu tofauti wanaweza kushirikiana na kukabiliana na fikra za watu wa kimagharibi ili kuondoa kasumba au tata zinazotolewa na watu hao kwa ajili ya kuiharifu, basi waislamu inawapasa  kuihifadhi dini yao na kutowaruhusu watu hao wenye fikra hizo mbovu kufanikiwa katika malengo yao ya kuiharibu dini hiyo takatifu.

Kwa hakika kuleta mashirikiano hayo kunahitajia kutunzwa au kuadhimishwa misingi na vigezo vya kila madhehebu, na jambo la muhimu zaidi ambalo linafaa kutekelezwa ni kuwa; kila dhehebu ni lazima litambue akida  ya dhehebu jengine, kwa sababu kufanya hivyo kunaweza kuzuia khitilafu zilizopo  baina ya dhehebu na dhehebu, na kupatikana njia zitakazoweza kuleta mashirikiano.1 2 3 4 5 6 7 8 9 next