IBADASisi tunaamini ya kwamba; fakhari kubwa ya Mitume na wajumbe wa Mwenyeezi Mungu ni kule wao kuwa watiifu kwa amri walizoamrishwa na Mola wao, na ni kwa sababu hiyo basi, sisi Waislamu siku zote katika sala zetu kuhusiana na Mtume Muhammad (s.a.w.w) tunakariri sentensi hii :-

واشهد ان محمد عبده ورسوله

Na nashuhudia ya kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ni mja na mjumbe wa

Mwenyeezi Mungu.

Sisi tuna itakidi ya kwamba; hakuna Mtume hata mmoja miongoni mwa Mitume ya Mwenyeezi Mungu aliyekuja na madai ya kuwa yeye ni mungu, na akawalingania watu kumuabudu yeye.

مَا كَانَ لِبَشَرٍ اَن يُؤْتِيَهُ اللّهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُواْ عِبَاداً لِّى مِن دُونِ اللهِ وَلَـكِن كُونُواْ رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ[19]

Haiwezi kuwa mtu aliye pewa na Mwenyezi Mungu Kitabu na hikima na Unabii kisha awaambie watu: Kuweni wa kuniabudu mimi badala ya Mwenyezi Mungu. Bali atawaambia: Kuweni wenye kumuabudu Mola Mlezi wa viumbe vyote, kwa kuwa nyinyi mnafundisha Kitabu na kwa kuwa mnakisoma.

Hata Nabii Issa pia hakuwalingania watu kumuabudu yeye, na siku zote alijitambulisha ya kuwa yeye ni mja aliyetumwa na Mwenyeezi Mungu.

لَّن يَسْتَنكِفَ الْمَسِيحُ اَن يَكُونَ عَبْداً لِّلّهِ وَلاَ الْمَلآئِكَةُ الْمُقَرَّبُونَ وَمَن يَسْتَنكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيهِ جَمِيعاً[20]

Masihi hataona uvunjifu kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu, wala Malaika walio karibishwa. Na watakao ona uvunjifu utumwa wa Mwenyezi Mungu na kufanya kiburi, basi atawakusanya wote kwake.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next