IBADASisi tunaamini ya kuwa; Mitume yote ya Mwenyeezi Mungu ni maasumu, (na umaasumu huo huwa nao kabla na baada ya kupewa utume), Mitume hao hawafanyi makosa wala maovu yoyote sio kwa kukosea wala kwa makusudi, kwa sababu kama watakuwa ni wenye kufanya makosa au uovu hakutakuwa na ulazima tena wa kupewa cheo hicho cha Utume, kwa sababu kwa kufanya hivyo, kutapelekea watu wasiwaamini Mitume hao kuwa wana uhusiano unaowafungamanisha nao na Mola Mtakatifu, na hawatoweza kuitambua Mitume hiyo kama ndio vigezo vyao katika maisha yao, au wahubiri wao wanaoweza kuwaongozaa katika njia ya saada.

Na kutokana na dalili hiyo basi, sisi tunaamini ya kwamba; ikiwa ndani ya Qur-ani mna Aya zinazomaanisha kuwa Mitume ya Mwenyeezi Mungu iliasi au kufanya maovu, kwa hakika hatuwezi kukubaliana au kuamini kuwa Mitume inaweza kufanya maovu, bali inawezekana tukasema kuwa waliacha yale yaliyo bora yaliyowalazimikia kuyatenda, (yaani baina ya mambo mawili mema walifanya moja ambalo sio bora zaidi kuliko lile jambo jengine), kauli hiyo tunakusudia kusema kuwa; Mitume ilichagua kutenda jema dogo, hali ya kwamba ilikuwa ni wadhifa wake kutenda lile jema kubwa na bora zaidi.

Kwa mfano kwa mtu wa kawaida sio jambo la lazima kwake kusali sala za usiku, lakini kwa upande wa Mitume, ni lazima kwao kusali sala ya usiku, kama pale aliposema Allah (s.w):-

يَا اَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ. قُمِ اللَّيْلَ إِلاَّ قَلِيلاً. نِصْفَهُ اَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلاً. اَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلاً
إِنَّا سَنُلْقِى عَلَيْكَ قَوْلاً ثَقِيلاً[17]

Ewe uliye jifunika! Kesha usiku kucha, ila kidogo tu! Nusu yake, au ipunguze kidogo . Au izidishe - na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo.

Hakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito.

Kwa hiyo inawezekana Mitume katika kuyafanya mambo mema mawili akachagua kufanya moja, hali ya kwamba ilimuwajibikia yeye kuyatenda yote mawili au kuchagua lile lililo bora zaidi, kwa hiyo hatuwezi kusema kuwa kutofanya hivyo ni uasi.

Kwa utaabiri mwengine tunaweza kusema hivi:-

"حسنات الابرار سیئات المقربین[18]

15. MITUME NI WAJUMBE WATIIFU WA MWENYEEZI MUNGU.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next