IBADA13. KUISHI PAMOJA NA WAFUASI WA DINI ZA ALLAH (S.W).

Ingawaje sisi Waislamu tuna itakidi ya kuwa dini ya Kiislamu ndiyo dini pekee iliyo rasmi katika zama hizi tulizonazo, lakini vile vile tunaamini ya kuwa ni lazima tuishi kwa salama na amani na wafuasi wa dini nyengine za Mwenyeezi Mungu, inawezekana wafuasi hao wakawa wanaishi katika nchi za Kiislamu, au pia wakawa hawaishi katika nchi za Kiislamu, isipokuwa kwa wale wanaopinga na kupiga vita dini ya Kiislamu.

لاَ يَنْهَاكُمُ اللهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِى الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ اَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ[15]

Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.

Sisi tunaamini ya kuwa; ikiwa dini ya Kiislamu itaarifishwa kimantiki, basi kutakuwa na uwezekano wa kuibainisha kwa uwazi dini hiyo kwa watu wote duniani, na kwa sababu dini ya Kiislamu ina dalili zenye nguvu na zinazokubalika kiakili na kimantiki basi kuna uwezekano wa kuwaongoa watu wengi duniani,, mahasusi katika dunia ya leo watu wengi wana kiu ya kusikia ujumbe wa dini ya Kiislamu.

Na ni kwa sababu hiyo basi, tunaitakidi kuwa hakuna ulazima wa kuwafosi watu kwa nguvu na kuwalazimisha ili kuingia katika dini hiyo kwa kuwalazimisha.

لاَ إِكْرَاهَ فِى الدِّينِ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ فَمَنْ يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَيَ لاَ انفِصَامَ لَهَا وَاللّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ[16]

Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Sisi tunaamini ya kuwa kuyatendea amali ri za dini ya Kiislamu inawezekana ikawa dalili bora nyengine inayoweza kuiarifisha dini ya Kiislamu bila ya kuiwepo haja ya kuwalazimisha watu au kuwafosi na kuwataka kuikubali dini hiyo.

14. MITUME NI MAASUMU KATIKA KIPINDI CHOTE CHA UMRI WAO.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next