IBADAرُّسُلاً مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلاَّ يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلـٰي اللهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ وَكَانَ اللّهُ عَزِيزاً حَكِيماً[11]

Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Sisi tuna itakidi ya kuwa; miongoni mwa Mitume hiyo, kuna Mitume mitano ambayo inajulikanwa kuwa ni “Uulil-Azmi” yaani ni Mitume iliyoteremshiwa vitabu vitukufu vya Mwenyeezi Mungu, Mtume wa mwanzo miongoni mwa Mitume hiyo mitano ni Nabii Nuhu (a.s), na baadae Nabii Ibrahimu (a.s), Nabii Mussa (a.s), Nabii Issa (a.s), na Mtume wa mwisho ambaye ni Nabii Muhammad (s.a.w.w).

وَإِذْ اَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَي وَعِيسَي ابْنِ مَرْيَمَ وَاَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقاً غَلِيظاً[12]

Na tulipo chukua ahadi kwa Manabii na kwako wewe, na Nuhu na Ibrahim na Isa mwana wa Mariamu, na tulichukua kwao ahadi ngumu,

فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ اُوْلُوا الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ وَلاَ تَسْتَعْجِل لَّهُمْ كَاَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَ مَا يُوعَدُونَ لَمْ يَلْبَثُوا إِلاَّ سَاعَةً مِّن نَّهَارٍ بَلاَغٌ فَهَلْ يُهْلَكُ إِلاَّ الْقَوْمُ الْفَاسِقُونَ[13]

Basi subiri, kama walivyo subiri Mitume wenye stahmala kubwa, wala usiwafanyie haraka. Siku watakayo yaona waliyo ahidiwa itakuwa kama kwamba hawakukaa ulimwenguni ila saa moja ya mchana. Huu ndio ufikisho! Kwani huangamizwa wengine isipo kuwa walio waovu tu?

Sisi tuna itakidi ya kuwa; Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndiye Mtume wa mwisho wa Mwenyeezi Mungu, na sheria na malinganio yake ni kwa ajili ya watu wote duniani, na sheria hizo zitabakia milele hadi mwisho wa dunia, kauli hiyo inathibitisha kuwa taaluma na hukumu zote za dini ya Kiislamu zinakidhi na kudhamini mahitajio yote ya wanaadamu, ya duniani na Akhera hadi mwisho wa dunia, kwa hiyo, mtu yeyote yule atakayekuja na madai ya kuwa yeye ni Mtume, basi madai hayo si ya kweli na yatakuwa hayana msingi wowote kwa wanaadamu.

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ اَبَا اَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَكِن رَّسُولَ اللهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ وَكَانَ اللهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيماً[14]

Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next