IBADAAma ni lazima tuzingatie kuwa; kauli hiyo haimaanishi kuwa kwa sababu hatuna elimu ya kuufahamu udhati wa ndani wa Mwenyeezi Mungu, basi vile vile hatuna elimu ya kumfahamu Mwenyeezi Mungu kijumla jamala, kwa hakika jambo hilo halikubaliki, kwa sababu Mwenyeezi Mungu ameviteremsha vitabu vyake ili kuwaletea wanaadamu elimu ya kumtambua Mola wao, na kwa kupitia vitabu hivyo wanaadamu huongoka na kufikia katika saada, tunaweza tukaashiria vitabu vingi kuhusiana na kauli hiyo, kwa mfano, sisi hatufahamu uhakika wa roho, ama kwa upande mwengine tuna elimu ya jumla jamala inayotuthibitishia kuwa roho ipo na tunaishuhudia.

Vile vile kuna hadithi maarufu iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Muhammad bin Aliy Baqir (a.s), yeye anasema:

کلما میزتموه بأوهامکم فی ادق معانیه مخلوق مصنوع مثلکم مردود الیکم[9]

Na katika hadithi nyengine iliyonukuliwa na Imamu Ali (a.s), hadithi ambayo inabainisha taaluma yake Allah (s.w):-

لم یطلع الله سبحانه العقول علی تحدید صفته و لم یحجبها امواج معرفته[10].

11.MWENYEEZI MUNGU HAJAFANANA NA KITU

Sisi tunaamini ya kuwa; kama tulivyo na itikadi ya kuwa kumfananiza Mwenyeezi Mungu na kitu ni jambo lisilokubalika, na atakayefanya hivyo atakuwa amemshirikisha Mwenyeezi Mungu, kwa upande mwengine ijapokuwa wanaadamu hawawezi kumtambua Mwenyeezi Mungu kwa udhati wake wote, lakini hii haimaanishi kuwa wanaadamu hatuna elimu hata kidogo ya kumtambua Mwenyeezi Mungu. Bali wanadamu wanaweza kumtambua Mola wao kwa kiwango kile cha elimu alichowajaalia.

KUPEWA UTUME KWA MITUME YA ALLAH (S.W).

12. FALSAFA YA KUPEWA UTUME MITUME YA ALLAH (S.W).

Sisi tuna amini ya kuwa ; Mwenyeezi Mungu amewateremsha Mitume yake ili kuwaongoza na kuwafikisha wanaadamu katika ukamilifu na saada, kama Mwenyeezi Mungu hakuwatuma Mitume kwa waja wake basi kusingelikuwa na hadafu wala madhumuni yoyote katika uumbaji wake, na wanaadamu wasingeliweza kuongoka na kufikia katika saada.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next