IBADA10. KINA CHA DHATI CHA UTAKASO WA ALLAH (S.W) KIMEFICHIKANA KWA WATU WOTE.

Sisi tuna amini ya kuwa; ijapokuwa athari ya kuwepo Mwenyeezi Mungu imeenea katika ulimwengu wote, lakini uhakika wa dhati ya Mwenyeezi Mungu ni jambo lisilo wazi kwa mwanaadamu yoyote yule, na hakuna mtu yeyote yule anayeweza kufahamu kina cha dhati ya Mwenyeezi Mungu, kwa sababu dhati yake Mola Mtakatifu haina mwisho, na imeizunguka kila kitu na sisi wanaadamu tuna mipaka maalumu, mipaka ambayo ina mwisho wake, na ni kwa sababu hiyo basi, sisi hatuwezi kuifikia dhati yake.

اَلاَ إِنَّهُمْ فِى مِرْيَةٍ مِّن لِّقَاء رَبِّهِمْ اَلاَ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُّحِيطٌ[6]

Ama wao wamo katika shaka ya kukutana na Mola wao Mlezi! Ama hakika Yeye amekizunguka kila kitu.

وَاللهُ مِن وَرَائِهِم مُّحِيطٌ[7]

Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka.

Katika hadithi maarufu ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) tunasoma, ya kuwa Nabii Muhammad (s.a.w.w) amesema:-

ما عبد ناک حق عبادتک وما عرفناک حق معرفتک[8]

Kwa hakika sisi hatujakuabudu Wewe vile unavyostahiki kuabudiwa, na

hatujakufahamu Wewe kwa uhaki, kama vile ilivyo haki yako kutambulika.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next