IBADAوَإِلَي ثَمُودَ اَخَاهُمْ صَالِحاً قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُواْ اللّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـهٍ غَيْرُهُ قَدْ جَاءتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ هَـذِهِ نَاقَةُ اللهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَاْكُلْ فِى اَرْضِ اللهِ وَلاَ تَمَسُّوهَا بِسُوَءٍ فَيَاْخُذَكُمْ عَذَابٌ اَلِيمٌ[3]

Na kwa Thamud tulimpeleka ndugu yao, Saleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika imekwisha kukufikieni Ishara iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye ni Ishara kwenu. Basi mwachieni ale kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimdhuru, isije kukushukieni adhabu chungu.

وَإِلَي مَدْيَنَ اَخَاهُمْ شُعَيْباً قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُواْ اللّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـهٍ غَيْرُهُ قَدْ جَاءتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ فَاَوْفُواْ الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ وَلاَ تَبْخَسُواْ النَّاسَ اَشْيَاءهُمْ وَلاَ تُفْسِدُواْ فِى الاَرْضِ بَعْدَ إِصْلاَحِهَا ذٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ[4]

Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Hamna mungu mwengine isipo kuwa Yeye. Imekwisha kufikieni hoja wazi kutoka kwa Mola Mlezi wenu. Basi timizeni sawasawa vipimo na mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika nchi, baada ya kuwa imekwisha tengenea. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini.

Jambo linalostaajabiosha ni kuwa waislamu siku zote katika sala zao wanazozisali wakati wanaposoma Surat hamd hukariri shairi hili muhimu la Waislamu lisemalo:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ[5]

Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada

Itikadi ya masuala ya shafaa ya Mitume na Malaika yaliyoelezewa katika Aya za Qur-ani, shafaa ambazo zitafanywa kwa aidhini yake Allah (s.w) kwa hakika haina maana ya ibada.

Na kuhusiana na Tawasuli ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, haina maana ya kuwa tawasuli hizo ni aina fulani ya ibada, au tawasuli inaendana sambamba na Tawhiyd katika matendo yake Allah (s.w). Bali Mitume humuomba Mola wao kuwaondolea waja wake mabalaa au matatizo mbali mbali, tutaielezea mada hiyo katika maudhui yanayohusiana na Mitume.

 

 back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next