IBADA
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

IBADA ZA WAJA WAKE MOLA MTAKATIFU.

Katika makala zilizopita tulielezea kuhusu itikadi za Shia Ithna Asharia, katika makala hii pia tutaendelea kuelezea itikadi nyengine za Shia Ithna Asharia.

9. IBADA ZOTE NI MAHASUSI KWA MOLA MTAKATIFU.

Kama tulivyoelezea katika mada inayohusiana na Tawhiyd katika ibada zake Allah (s.w) kuwa ibada zote zinazofanywa na waja ni lazima ziwe mahasusi kwa ajili ya Allah (s.w) tu, kwa hiyo mtu yeyote yule atakayeabudu isiye Mwenyeezi Mungu, basi mtu huyo atakuwa ni miongoni mwa washirikina, na malinganio ya Mitume yote ilisisitiza kauli hiyo. na katika Qur-ani kuna aya tofauti zilizokariri kauli hiyo.

لَقَدْ اَرْسَلْنَا نُوحاً إِلَي قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُواْ اللهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـهٍ غَيْرُهُ إِنِّيَ اَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ[1]

Tulimpeleka Nuhu kwa kaumu yake, naye akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku iliyo kuu.

وَإِلَي عَادٍ اَخَاهُمْ هُوداً قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُواْ اللّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـهٍ غَيْرُهُ اَفَلاَ تَتَّقُونَ[2]

Na kwa A'adi tulimpeleka ndugu yao, Hud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi?1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next