NAFSI YA DINI NDANI YA JAMIIMaelezo kuhusiana na aya:

*Watakuwa na uhai mzuri kwa sababu, kila mtu atakaa kwa adabu yake, kwani anajua kuwa akiua atauawa, na akidhuru na yeye atafikishiwa madhara. Katika kujikimbizia madhara nafsi yake yanakimbizika hayo madhara ya watu wengine

*“Alqisas hayat” yaani ndani ya kisasi pia mna maisha, hivyo katika kisasi watu wanaweza wakafanya suluhu au kusameheana.

Katika maelezo yaliyopita tulielezea aina za dini, katika sehemu hii tutaelezea kwa kina zaidi aina hizo za dini.

Dini zimegawika katika sehemu mbili:-

1.Dini zinazotokana na kizazi cha Nabii Ibrahimu (a.s), dini hizo ndizo dini za Allah (s.w).

2. Dini zinazotokana na tamaduni maalumu za watu, dini hizo sio dini sahihi.

Dini ya wahyi ni dini ya Nabii Ibrahimu (a.s) na ndio dini iliyoletwa kutoka kwa Mwenyeezi Mungu Mtukufu. ni bayana maalumu inayowafunga watu wote katika mfumo mmoja, na katika mwenendo maalumu, na inawalazimu wao kuitii dini hiyo.

Wahyi wa dini ni wenye kukubalika na kufahamika katika tamaduni zote, hii ni kwa sababu wahyi huo unawiana na kuwendana na matakwa ya dini, matakwa ya dini ni matakwa ya wanaadamu wote, ikiwa dini inakubalika na kufahamika na wanaadamu wote, na ikiwa dini ina uwezo wa kufuta, na kuondoa mambo yanayoleta madhara na yasiyo na faida yoyote katika maisha ya mwanaadamu, au inaweza kuweka na kuwaletea wanaadamu maadili mema yaliyo na faida katika maisha yao, na yanayowaletea saada ya duniani na Akhera, hii ni kwa sababu lugha ya dini ni lugha iliyomo ndani ya nafsi za wanaadamu wote , na ni lugha inayofahamika na kila mmoja wetu, na ni lugha inayowaletea wanaadamu athari nzuri katika maisha yao.

Lugha mahasusi na maalumu ya dini ni lugha ya kiarabu, lugha ya nafsi, na ni lugha asili iliyojaaliwa kutokana na mambo yote yaliyo dhahiri na yaliyo jificha, mambo ambayo yana uhusiano na ulimwengu wa wanaadamu.back 1 2 3 4 5 6 7 8 next