NAFSI YA DINI NDANI YA JAMIIKumerushwa tata inayosema kuwa dini imeteremshwa kwa mujibu wa utamaduni wa watu, Au kwa maana nyengine dini haiteremshwi bila ya kuwepo utamaduni.

Hivi kweli kauli hiyo ni sahihi? Ili kuipatia jawabu tata hiyo naturejee katika historia ya dini na chanzo chake. Kwa ufupi tunaweza kuijibu tata hiyo kwa kusema:-

Dini ndio iliyovumbua tamaduni, na sio tamaduni zimevumbua dini, kwa hiyo utamaduni umo ndani ya dini, na sio dini imo ndani ya utamaduni, dini kwa mwanaadamu ni fitra yaani (nature)- religion is nature from the God -. Dini ndio iliyokuja kuwafundisha wanaadamu maadili mema, na kupinga maadili mabaya yaliyokuwa yakifanywa na makafiri na washirikina, na sio utamaduni wa baadhi ya watu ndio uliokuja kuwafunza watu umuhimu wa dini au maadili mema, katika sehemu hii natuangalie baadhi ya mambo mabaya yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya watu, vikundi au makabila, mambo ambayo yamesawazishwa na kutengenezwa kupitia dini takatifu ya Allah (s.w).

Miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo:-

- kukataza kuabudu masanamu, na kuabudu Mola mmoja mtakatifu

- kusahihisha ibada ya tawafu, baadhi ya watu walikuwa wakitufu hali ya kuwa wako uchi bila ya nguo, dini imesawazisha na kuwataka watufu kwa mujibu wa misingi maalumu.

- Mauaji ya kabila na kabila:

Baadhi ya wakati makabila yalikuwa yakikhitilafiana, au kabila moja kuuwa mtu wa kabila jengine, kabila la mtu aliyeuliwa lilikuwa likitoka na kwenda kulipiza kisasi kwa watu wote wa kabila hilo, na si kuuwa mtu mmoja tu ambaye amemuuwa mtu fulani, dini imesawazisha na kuwaambia :-

وَلَكُمْ فِى الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَاْ اُولِيْ الاَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ[5]

Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike.back 1 2 3 4 5 6 7 8 next