NAFSI YA DINI NDANI YA JAMIIYeye (s.w) anasema:-

" وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لاَ يَعْلَمُهَا إِلاَّ هُوَ وَيَعْلَمُ مَا فِى الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلاَّ يَعْلَمُهَا وَلاَ حَبَّةٍ فِى ظُلُمَاتِ الاَرْضِ وَلاَ رَطْبٍ وَلاَ يَابِسٍ إِلاَّ فِى كِتَابٍ مُّبِينٍ[3]".

Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinachobainisha.

Maana na ufafanuzi wa Aya hiyo ni kama ifuatavyo:-

Vitu vyote duniani vilivyo na uhai na visivyo na uhai vimedhibitiwa ndani ya Qur-ani na viko katika milki yake Yeye Allah (s.w), yaani rikodi ya kila kitu iko kwa Allah (s.w).

Kuwepo kwa Qur-ani kwa ajili ya dini ya Kiislamu, na pasitokee na mtu yoyote atakayeweza kukiharibu au kukiharifu kitabu hicho, yote hayo yanathibitisha uwezo wake Allah (s.w) katika kuihifadhi dini na kitabu chake kitukufu. Ikiwa patatokea mtu awezae kuipunguza au kuizidisha herufi angalau moja ya Qur-ani (na hakuna anayeweza wala atakayeweza kufanya hivyo) basi kitabu hicho hakitakuwa kitabu cha Wahyi wa Mwenyeezi Mungu, wala hakitakuwa kitabu cha dini.

Ufafanuzi wa paragrafu hiyo ni kwamba:-

Mwenyeezi Mungu amekiteremsha kitabu cha Qur-ani kikiwa ni nyenzo ya kumuongoza mwanaadamu katika saada kwa kufanya yale aliyoamrishwa na Mola wake kupitia kitabu hicho, na kwa muongozo wa Mitume ya Mwenyeezi Mungu na Ahlulbayt (a.s), kwa hiyo kama tukisema kuwa kitabu hicho kina upungufu au kimezidishwa baadhi ya mambo ambayo Mwenyeezi Mungu hakuyatia mambo hayo katika kitabu hicho, itamfanya mwanaadamu awe na udhuru wa kumshitakia Mola wake kuwa yale aliyomtaka ayafanye yalizidishwa au kupunguzwa katika kitabu hicho ambacho kilikuwa ndio muongozo wake.

Tunaweza kuufafanua ufumbuzi wa dini katika njia mbili zifuatazo:-

1. kwa kuifanyia uhakiki nafsi ya mwanaadamu mwenyewe.back 1 2 3 4 5 6 7 8 next