NAFSI YA DINI NDANI YA JAMII(2). Dini ya kisheria.

Dini ni miongozo, pamoja na amri zenye kuuelekea ulimwengu na walimwengu kimaumbile na kisheria, amri za kisheria zina uhuru wa kutenda au kutotenda, isipokuwa tu uhuru huo haumaanishi kwamba wewe umeachiwa utende utakavyo, kwa hiyo utendekaji wa amri za kisheria unahitajia msukumo na jitihada za mwanaadamu, ikiwemo hiyari ya mwanaadamu katika utendekaji wa sheria, na hii ndio sharti kuu ya kufanya kitendo akifanye atakavyo, na muhusika mkuu ni mwanaadamu.

Ama katika amri za kimaumbile muhusika mkuu ni Allah (s.w), kwani amri za kimaumbile na zile sifa na nyenendo maalumu za kimaumbile zenye msukumo wa kimaumbile usiohitajia hiyari, bali inawezekana kukawepo baadhi ya nyenendo za kimaumbile ambazo mwanaadamu anaweza kuzizuia na kuzipeleka katika njia nyengine kwa kiasi fulani, huku Mitume wakionekana kuwa na nguvu za moja kwa moja katika kuzisarifu zile nyenendo zote za kimaumbile kwa adhini ya Mola Mtakatifu.

1. Kwa hiyo, dini ni kitu ambacho uhakika wake tayari uko wazi na ni wenye kutambulika, uhakika ambao umekusanya ndani yake mfumo mzima wa maisha ya mwanaadamu kijumla jamala, na sio kwa ajili ya kikundi au watu maalumu.

 Sio jambo lenye kukubalika kuwa dini ni fikra maalumu za watu, wawe wanasiasa au wana elimu mbali mbali, kwa hiyo ni Mwenyeezi Mungu tu anayeweza kutengeneza dini, na dini tayari imeshatengenezwa kwa mujibu wa maisha na mahitajio ya wanaadamu, ni jambo lilsiloingilika akilini kuwa watu waende kutafuta dini, kwa sababu dini iko tayari, na ni wadhifa wa kila mwanaadamu kufuata dini na sio kutengeneza, mfumo wa haki wa dini ni wa Allah (s.w) na sio watu wengine. Natija tunayoipata kutokana na maelezo hayo ni kuwa :-

*Dini ni mjengeko uliopangwa kwa nidhamu maalumu katika kipindi chote cha tarehe, kuanzia wakati alipoumbwa mwanaadamu hadi zama hizi tunazokwenda nazo, dini imetumwa kwa watu kwa ajili ya kuwapa uwezo wa kufahamu mambo mbali mbali yanayohusiana na maisha yao, na mambo mengine yote, dini ambazo zimekuja kwa mujibu wa fikra au mifumo ya wanaadamu hizo sio dini za Mwenyeezi Mungu na dini hizo zitakuwa ni nakisi na zenye upungufu, kwa hiyo dini hizo sio sahihi.

Ikiwa patatokea – mbali na Mitume na Ahlulbayt- mtu atakayekuja na madai au ujumbe wa kudai kuwa ujumbe huo amepewa na Mwenyeezi Mungu, au ana uhusiano fulani na Mwenyeezi Mungu basi mtu huyo hana dini, na hana mfumo wowote unaonasibiana na mfumo wa dini aliyoileta Mwenyeezi Mungu (s.w).

Dini ni mfumo na mjengeko uliopangwa kwa nidhamu maalumu, kwa ajili ya watu wote duniani katika kipindi chote cha tarehe ya binaadamu, Mwenyeezi Mungu ameitengeneza dini na kuwapelekea waja wake kulingana na mahitajio yao ya kila siku, kuanzia zama za Nabii Adam (a.s) hadi zama atakazodhuhuru kiongozi muokozi wa Waislamu, hadharati Mahdi Ajjala llahu Taala Sharifu.

Dini ni mfumo maalumu wa elimu, hukumu, na taaluma mbali mbali za kitabu kitukufu cha Wahyi wa Mwenyeezi Mungu (Qur-ani) , ndani ya kitabu hicho kuna mabainisho mbali mbali ya mambo yaliyopita, mambo yaliyopo, yajayo na mambo yatakayokuja, ndani ya kitabu hicho mna kila kitu anachokihitajia mwanaadamu na viumbe wote kwa ujumla cha dhahiri na cha batini. Natuangalie Aya hii tukufu ya Mwenyeezi Mungu iliyonukuliwa na mmoja wa Maimamu maasumu (a.s) Yeye kuhusiana na dini anasema hivi:-

Funguo za kila elimu ziko kwake Yeye Mola Mtakatifu, na anayathibitisha hayo kupitia kauli yake Allah (s.w)back 1 2 3 4 5 6 7 8 next