NAFSI YA DINI NDANI YA JAMIINguo ya dini inaendana sawa na Uislamu, na Uislamu unawafunga watu katika mfumo mmoja.

Na kwa sababu neno “ISLAM” kijumla lina maana ya kusalimu amri (kusarenda) katika amri, sheria, kanuni na hukumu zote alizoamrisha Mwenyeezi Mungu. (hukumu za kimaumbile na hukumu za kisheria) . Kwa hiyo, kwa kuzingatia maana ya neno Islam, ni lazima maana ya neno dini liwiane na maana hiyo.

Ni jambo lililowazi kabisa kuwa, haiwezekani kulitumia neno dini katika maana yake ya kijumla, na kulitumia neno hilo kwa kulipa maana maalumu, kwa sababu neno dini limetumika katika sehemu tofauti likiwa na maana tofauti. maana ya kijumla ya neno dini inaweza kutafsiriwa katika mambo mbali mbali, kwa mfano, tunaweza kusema dini ya kikafiri, au dini ya washirikina, n.k. hiyo ni kwa mtazamo wa kijumla, lakini neno dini katika maana yake maalumu inakusudiwa dini ya Kiislamu, na hii ndio maana sahihi.

Neno dini, na neno Islam, linashabihiana na kuwiana katika maana zake, tukijaalia kuwa sadikisho la dini ni Islam, basi tunaweza kulifafanua neno dini katika mtazamo wa kitaalamu kwa kusema :-

Dini ni mkusanyiko wa desturi, mabainisho, maamrisho ya kimaumbile na ya kisheria, yanayowafungamanisha watu katika mfumo mmoja kulingana na mahitajio ya vitu vyote ulimwenguni, wanaadamu, mimea, wanyama n.k. yote hayo yametumwa na Mwenyeezi Mungu kupitia Mitume na Ahlulbayt wake kwa ajili ya kuwapelekea wanaadamu na viumbe vyote kijumla .ili waifikie saada katika maisha yao ya  duniani na Akhera .

Kwa ubainisho mwengine tunaweza kusema hivi:-

Dini ina maana moja tu, nayo ni Islamu, na kuna njia mbili za dini:-

(1). Dini ya kimaumbile, kama anavyosema Allah (s.w):-

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ وَإِذَا قَضَي اَمْراً فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ[2]

 Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina ruwaza; na anapotaka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa.back 1 2 3 4 5 6 7 8 next