KUMTAMBUA MOLA MLEZINa pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu!

Na kuhusiana na mmoja wa Mawaziri wa nabii Suleiman (a.s) tunasoma:-

قَالَ الَّذِى عِندَهُ عِلْمٌ مِّنَ الْكِتَابِ اَنَا آتِيكَ بِهِ قَبْلَ اَن يَرْتَدَّ إِلَيْكَ طَرْفُكَ فَلَمَّا رَآهُ مُسْتَقِرّاً عِندَهُ قَالَ هَذَا مِن فَضْلِ رَبِّى لِيَبْلُوَنِى اَاَشْكُرُ اَمْ اَكْفُرُ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّى غَنِيٌّ كَرِيمٌ[17]

Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu.

Kwa hiyo muujiza wa Nabii Issa (a.s) ulioelezewa ndani ya Qur-ani, wa kuwapa watu shafaa kutokana na magonjwa waliyokuwa nayo, magonjwa ambayo hakukuwepo uwezekano wa kuyatibu, au kuwafufua waliokufa, yote hayo aliyafanya Nabii Issa kwa adhini yake Allah (s.w), basi hayo pia ni miongoni mwa Tawhiyd yake Allah (s.w).

8. MALAIKA WAKE ALLAH (S.W).

Sisi tuna itikadi ya kuwepo kwa Malaika wa Mwenyeezi Mungu, na kila Malaika ana majukumu yake aliyopangiwa na Mola wake, baadhi ya Malaika wana wadhifa wa kupeleka Wahyi wa Mwenyeezi Mungu kwa Mitume

قُلْ مَن كَانَ عَدُوّاً لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلـٰي قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللهِ مُصَدِّقاً لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَي لِلْمُؤْمِنِينَ[18]

Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

Na baadi yao wana wadhifa wa kuhifadhi amali na matendo ya wanaadamu.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 next