KUMTAMBUA MOLA MLEZIIli mwanaadamu afikie katika hatua ya ukamilifu wa kitabia kiamali na kimatendo ni lazima aikurubishe na kuifunga nafsi yake na Mola wake, amtegemee Mola wake katika kila kitu, na asighafilike na kitu chochote kile kitakachomfanya yeye awe mbali na Mola wake, کلما شغلک عن الله فهو صنمک

Yaani kitu chochote kile kinachomghafilisha mwanaadamu na kumuweka mbali na Mwenyeezi Mungu basi ndio sanamu lake.

Sisi tuna itikadi ya kuwa Tawhiyd haijafungika katika matawi hayo manne tu, bali pia kuna tawi la Tawhiyd katika milki na ufalme wake Allah (s.w), (yaani vitu vyote viko katika milki yake Mwenyeezi Mungu).

للَّهِ ما فِى السَّمَاواتِ وَمَا فِى الاَرْضِ وَإِن تُبْدُواْ مَا فِى اَنفُسِكُمْ اَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ اللّهُ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَاللّهُ عَلـٰي كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ[14]

Viliomo mbinguni na viliomo duniani ni vya Mwenyezi Mungu. Na mkidhihirisha yaliyomo katika nafsi zenu au mkayaficha, Mwenyezi Mungu atakuhisabuni kwayo. Kisha amsamehe amtakaye na amuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

Vile vile kuna tawi la Tawhid linalojulikana kwa jina la Tawhiyd katika hekima zake Allah (s.w). yaani kila kanuni na kila sheria ni zake Yeye Mola mtakatifu.

إِنَّا اَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ اَسْلَمُواْ لِلَّذِينَ هَادُواْ وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالاَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُواْ مِن كِتَابِ اللهِ وَكَانُواْ عَلَيْهِ شُهَدَاء فَلاَ تَخْشَوُاْ النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلاَ تَشْتَرُواْ بِآيَاتِى ثَمَناً قَلِيلاً وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا اَنزَلَ اللّهُ فَاُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ[15]

Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.

7. Sisi tuna itakidi ya kuwa; msingi na asili ya Tawhiyd unathibitisha ya kuwa miujiza yote iliyofanywa na Mitume ya Mwenyeezi Mungu imefanywa kwa idhini yake Allah (s.w), kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani kuhusiana na Nabii Issa (a.s):-

إِذْ قَالَ اللّهُ يَا عِيسى ابْنَ مَرْيَمَ اذْكُرْ نِعْمَتِى عَلَيْكَ وَعَلـٰي وَالِدَتِكَ إِذْ اَيَّدتُّكَ بِرُوحِ الْقُدُسِ تُكَلِّمُ النَّاسَ فِى الْمَهْدِ وَكَهْلاً وَإِذْ عَلَّمْتُكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالإِنجِيلَ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ بِإِذْنِى فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْراً بِإِذْنِى وَتُبْرِئُ الاَكْمَهَ وَالاَبْرَصَ بِإِذْنِى وَإِذْ تُخْرِجُ الْمَوتَي بِإِذْنِى وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِى إِسْرَائِيلَ عَنكَ إِذْ جِئْتَهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُواْ مِنْهُمْ إِنْ هَـذَا إِلاَّ سِحْرٌ مُّبِينٌ[16]back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 next