KUMTAMBUA MOLA MLEZINa ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe?

Aya hiyo inaonyesha kwa uwazi kabisa kuwa mwanaadamu ni mwenye uhuru na anayeweza kufanya ayatakayo, lakini kwa sababu uhuru huo alionao mwanaadamu ameupata kutokana na Qudra na nguvu zake Allah (s.w), kwa hiyo tuna majukumu na wadhifa katika amali na matendo yetu tunayoyafanya, hivyo ni lazima tuwe na mazingatio katika matendo yetu na kufanya yale ambaye Allah (s.w) ametuamrisha.

Ndio, Mwenyeezi Mungu ametuwacha huru tufanye matendo na amali zetu kwa hiyari zetu, ili kutufanyia mtihani, kwani pindi tukifanya matendo yetu kwa uhuru, kupitia njia hiyo tunaweza kufikia katika ukamilifu, kwa sababu ni uhuru peke yake ndio utakaomfanya mwanaadamu aweze kumtii Mola wake kwa hiyari yake, bila ya kulazimishwa au kufosiwa, kwani mwanaadamu kufanya amali kwa kulazimishwa sio dalili nzuri itakayomfikisha mwanaadamu katika ukamilifu.

Ikiwa mwanaadamu atalazimishwa katika kufanya amali na matendo yake basi kulikuwa hakuna umuhimu wowote wa kuteremshwa Mitume wala kuteremshwa vitabu, vitabu ambavyo Mwenyeezi Mungu ameviteremsha kwa waja wake ili kuwaongoza katika njia njema, na wala kungelikuwa hakuna maana ya malipo ya jazaa njema au adhabu kali iumizayo.

Basi kutokana na maelezo ya Maimamu na Ahlulbayt (a.s) kuwa:

لاجبر ولا تفویض ولکن امر بین امرین[12]

D: TAWHIYD KATIKA IBADA ZAKE ALLAH (S.W)

Mwenyeezi Mungu pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa, na hakuna yeyote anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye Allah (s.w),  tawi hilo la Tawhiyd ndiyo tawi muhimu miongoni mwa matawi ya Tawhiyd, na Mitume ya Mwenyeezi Mungu ilitegemea na kuzingatia zaidi aina hiyo ya Tawhiyd.

وَمَا اُمِرُوا إِلاَّ لِيَعْبُدُوا اللهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاء وَيُقِيمُوا الصَّلاَةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ وَذٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ[13] 

Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 next