KUMTAMBUA MOLA MLEZIYaani athari ya kila tendo, na kila harakati inayoshuhudiwa duniani, inatokana na idhini na matakwa yake Allah  (s.w)

اللهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ عَلـٰي كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ[8]

Mwenyeezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu.

لَهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ[9]  

Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu.

Ndio, “لا مؤثر فی الوجود الا الله”.

Lakini kauli hiyo haimaanishi kuwa sisi hatna hiyari katika matendo yetu tunayoyafanya, bali tuko huru katika maamuzi na matendo yetu tunayoyafanya.

إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِراً وَإِمَّا كَفُوراً[10]

Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.

وَاَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلاَّ مَا سَعَي[11]back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 next