KUMTAMBUA MOLA MLEZINa kwa yakini yamefunuliwa kwao, na kwa wale waliokuwa kabla yako (maneno haya):- kama ukimshirikisha (Mwenyeezi Mungu) bila ya shaka amali zako zitaruka patupu, (hutazipata thawabu japo ni amali njema), na lazima utakuwa miongoni mwa wenye hasara.

6. MATAWI YA TAWHIYD.

Sisi tuna itikadi ya kuwa tawhiyd ina matawi mbali mbali, na kuna manne muhimu miongoni mwa hayo, nayo ni haya yafuatayo:-

A: TAWHIYD KATIKA DHATI YAKE ALLAH (S.W).

Yaani dhati ya Allah (s.w) ni moja, naye ni mmoja tu, asiyefanana na kitu chochote ulimwenguni.

 

 

B: TAWHIYD KATIKA SIFA ZAKE ALLAH (S.W).

Tawhiyd katika sifa za Mwenyeezi Mungu, yaani sifa zote za Mwenyeezi Mungu, mfano elimu, Qudra na uwezo, ubakiaji wa milele wa Allah (s.w), na sifa nyengine nyingi zote ziko katika dhati yake Allah (s.w), sio kama sifa za viumbe, kwani sifa za viumbe haziko ndani ya udhati wa viumbe bali ziko nje ya viumbe, ama ni lazima tuzingatie kuwa; dhati hiyo ya sifa za Mwenyeezi Mungu inahitajia tafakuri na mazingatio ya kifikra.

C: TAWHIYD KATIKA MATENDO YAKE ALLAH (S.W).back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 next