KUMTAMBUA MOLA MLEZIKwa hakika Qur-ani inafasiri baadhi ya Aya nyengine.

Mbali ya hayo, tukiongezea kuithibitisha kauli hiyo, Imamu Aliy (a.s) alipokuwa akijibu suala la mmoja wa wafuasi wake, pale alipoulizwa:

یا امیر المؤمنین هل رأیت ربک.   yaani, Ewe Amiyrul-Muuminiyna, hivi kweli umewahi kumuona Mola wako? Imamu Aliy (a.s)  akamjibu  kwa kumwambia: أأعبد مالا اری ; yaani, hivi kweli nitaabudu nisiyemuona?. baadae akaendelea kwa kusema:-

" لا تدرکه العیون بمشاهدة العیان. ولکن تدرکه القلوب بحقایق الایمان[5] "

Macho katu hayawezi kumuona Mwenyeezi Mungu kwa uwazi, lakini nyoyo na nafsi za wanaadamu kwa kutumia nguvu za imani zinaweza kumuona Allah (s.w).

Sisi tuna itikadi ya kuwa; Kumnasibisha Mwenyeezi Mungu kwa sifa za viumbe, kama mwenyeezi Mungu kuwa na sehemu au zama maalumu, kuwa ana kiwiliwili, au kuwa na itikadi ya kuwa Mwenyeezi Mungu anaweza kushuhudiwa kwa macho, husababisha kuwa mbali na taaluma au elimu ya kumtambua Mwenyeezi Mungu, na mwenye na itikadi hizo basi atakuwa amemshirikisha Mwenyeezi Mungu, ndio Mwenyeezi Mungu (s.w) ni mbora wa kila kitu, na mbora wa kila sifa, na hakuna kitu chochote kinachofanana na Yeye.

5. TAWHIYD NI KIINI CHA ELIMU NA MAFUNZO YOTE YA UISLAMU.

Sisi tuna itakidi ya kuwa; mambo muhimu yanayohusiana na elimu na taaluma bora ya Mwenyeezi Mungu ni Tawhiyd, na kuwa na imani ya kuwepo Mola mmoja aliyetakasika, kwa hakika Tawhiyd sio msingi miongoni mwa misingi ya dini tu, bali, mbali ya kuwa Tawhiyd ni msingi wa dini vile vile ni kiini cha itikadi zote za Kiislamu, na tunaweza kusema kuwa; Misingi na matawi ya Kiislamu  yamejikusanya katika misingi ya Tawhiydi, kila kipengele miongoni mwa vipengele vya Islamu kumezungumzwa masuala ya Tawhid, na kuwa na imani na Mola mmoja, tawhiydi katika sifa na matendo ya Mwenyeezi Mungu, Tawhiyd katika malengo mamoja walikuja nayo Mitume walipokuwa wakilingania nyumati zao, Tawhiyd katika dini moja miongoni mwa dini za Mwenyeezi Mungu, Tawhiydi katika kibla na vitabu vya mwenyeezi Mungu, Tawhitdi katika hukumu na sheria za Mwenyeezi Mungu kwa wanaadamu wote, na hatimae Tawhiyd kwa Waislamu wote na tawhiyd kwa siku ya Kiama, na kwa sababu hiyo basi, Qur-ani takatifu inabainisha kuwa upotoshaji wowote ule utakaofanywa katika tawhiyd ya Mwenyezi Mungu ni uovu usiosamehewa na ni shirki kubwa.

إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ اَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ وَمَن يُشْرِكْ بِاللهِ فَقَدِ افْتَرَي إِثْماً عَظِيماً[6]
Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa.

وَلَقَدْ اُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَي الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكَ لَئِنْ اَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ[7]back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 next