KUMTAMBUA MOLA MLEZIEnyi mlio amini! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu. Pale yalipo kufikilieni majeshi, nasi tukayapelekea upepo, na majeshi msiyo yaona. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.

Na baadhi ya Malaika wana wadhifa wa kuwalipa adhabu kaumu na watu walio muasi Mwenyeezi Mungu. na mbali ya majukumu hayo, vile vile wana majukumu mengine katika nidhamu ya uumbaji wa dunia.

وَلَمَّا جَاءتْ رُسُلُنَا لُوطاً سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعاً وَقَالَ هَـذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ[23]

 Na wajumbe wetu walipo kuja kwa Lut' aliwahuzunukia na akawaonea dhiki. Akasema: Hii leo ni siku ngumu!.

Hakuna shaka ya kuwa majukumu yao huyatekeleza kwa idhini ya Mola wao, basi nyadhifa hizo zinasisitiza na kuendana sambamba na misingi ya kimatendo ya Tawhiyd, kwa kuzingatia kwa makini maelezo hayo, tutafahamu kuwa masuala ya shafaa ya Mitume na Malaika hutekelezwa kwa idhini ya Mola Mtakatifu,

إِنَّ رَبَّكُمُ اللّهُ الَّذِى خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضَ فِى سِتَّةِ اَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَي عَلـٰي الْعَرْشِ يُدَبِّرُ الاَمْرَ مَا مِن شَفِيعٍ إِلاَّ مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ذٰلِكُمُ اللّهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ اَفَلاَ تَذَكَّرُونَ[24]

Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha mambo yote. Hapana mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki?

maelezo kuhusiana na masuala ya shafaa na tawasuli tutayaelezea kwa kina katika mada inayohusiana na Mitume.[1] Surat Al-An-aam Aya ya 103

[2] Suratul-Baqarah Aya ya 55back 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 next