KUMTAMBUA MOLA MLEZI
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

KUMTAMBUA MWENYEEZI MUNGU

Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu itikadi ya Shia Ithna Asharia, katika makala hiyo tulielezea baadhi tu ya akida na yale wanayoamini wafuasi wa madhehebu ya Shia Ithna Asharia. Katika makala hii tutaendelea kubainisha itikadi nyengine za watu wa madhehebu ya Shia.

Miongoni mwa itikadi nyengine za Shia Ithna Asharia ni kuwa, wao wanaamini kwamba Mwenyeezi Mungu sio kiumbe na wala haiwezekani Yeye kufananizwa na kitu chochote.

4. MWENYEEZI MUNGU SI KIUMBE, HANA KIWILIWILI NA KATU HAONEKANI.

Sisi tuna imani ya kuwa; Mwenyeezi Mungu haonekani kwa macho katu, kwa sababu kuona kwa macho kunamaanisha kuwa Mwenyeezi Mungu ni kiumbe aliye na kiwiliwili, aliye katika sehemu maalumu, au umbo maalumu, hali ya kwamba sifa hizoo ni sifa za viumbe vilivyoumbwa na Mwenyeezi Mungu, hali ya kwamba ubora na utukfu wa sifa za Mwenyeezi Mungu uko juu zaidi, kiasi ya kwamba haiwezekani kumfananisha Yeye na sifa za viumbe, kwa hivyo hatuwezi kumsifu Mwenyeezi Mungu kwa sifa za viumbe vyake, kwa hiyo kuwa na itikadi ya kumuona Mwenyeezi Mungu sio sahihi, na itikadi hiyo ni miongoni mwa aina fulani za shirki, na huko ndio kumshirikisha Mwenyeezi Mungu, Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:-

لاَّ تُدْرِكُهُ الاَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الاَبْصَارَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ[1]

Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari.

Na ni kwa dalili hiyo basi, kaumu ya Bani Israili ikatoa hoja kumwambia Nabii Mussa (a.s) kuwa hawatamuamini Mwenyeezi Mungu isipokuwa pale watakapomuona, pale waliposema:-1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 next