UONGOZI KATIKA ZAMA ZA IMAMU ALI (A.S)
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UONGOZI WA IMAMU ALI (A.S)

YANAYOHUSIANA NA HUZUNI NA MJUTO

Kama kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka Wilayah ya Ali iwe ni mtihani kwa Waislamu, basi kila ikhtilafu iliyotokea imekuwa ni kwa sababu ya Wilayah hiyo, naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mpole kwa waja wake, hawezi kuwaadhibu waliokuja baadaye kwa makosa yaliyofanywa na wale wa mwanzo. Kwa ajili hiyo imetukuka hekima yake, tukio hili la ukhalifa likazungukwa na mfululizo wa matukio mengine makubwa yafananayo na miujiza, ili iwe ni kichocheo kwa umma. Waliinakili hali hii waliokuwepo ili wapate mazingatio wajao baadaye huenda wakaongoka na kuelekea kwenye haki kwa njia ya kufanya utafiti.

Ushahidi wa Kwanza:

Unafungamana na adhabu kwa wale waliokadhibisha Wilayah ya Ali, hilo lilitokea baada ya kuenea kwa habari za Ghadir Khum na kusimikwa kwa Imam Ali kuwa ni Khalifa wa Waislamu kutokana na kauli ya Mtume alipowaambia "Aliyeshuhudia tukio hilo amfikishie habari asiyehudhuria ".

Habari hizo za tukio la Ghadir zilimfikia Harith bin Nuuman Al-Fihri na hakufurahishwa na habari hizo- Hapa kuna dalili kwamba walikuwepo Mabedui waliokuwa wakiishi nje ya Madina ambao walikuwa wakimchukia Ali na pia Mtume (s.a.w.w). Basi huyu bwana alimsimamisha mnyama wake mbele ya mlango wa msikiti akaingia kwa Mtume (s.a.w.w) akasema: "Ewe Muhammad bila shaka wewe umetuamuru tushuhudie kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, tumekukubalia hilo, na umetuamuru tusali mara tano kwa siku, tufunge Ramadhan, Tuhiji na tutoe zaka mali zetu tukakukubalia, kisha hukuridhika kwa haya mpaka umeinyanyua mikono ya mwana wa ammi yako na umemboresha juu ya watu ukasema:

"Yeyote ambaye mimi ni mtawalia mambo yake basi Ali ni mtawalia mambo yake". Jambo hili latoka kwako au latoka kwa Mwenyezi Mungu"?

Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema hali ya kuwa macho yake yamekuwa mekundu: "Namuapa Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mola isipokuwa yeye, jambo hilo latoka kwa Mwenyezi Mungu na halitoki kwangu" Akasema maneno hayo mara tatu.!!

Harith alisimama huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa ayasemayo Muhammad ni ya kweli, basi tuletee mawe toka mbinguni au utuletee adhabu kali".1 2 3 next