HASARA NA MAJUTO
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

YANAYOHUSIANA NA HASARA NA MAJUTO KWA WAISLAMU

Kwa nini nisijute; bali ni kwa nini kila Muislamu asijute wakati usemwapo ukweli huu unaoelezea hasara waliyoipata Waislamu kutokana na kutengwa kwa Imam Ali kwenye Ukhalifa ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtawalisha, na hivyo kuunyima umma (wa Kiislamu) uongozi wake na hekima, na elimu yake nyingi.

Na pindi Muislamu atakapochunguza bila ya chuki wala upendeleo, atamkuta Imam Ali ndiyo mwenye elimu na mjuzi mno kuliko watu wote baada ya Mtume, kwani tunashuhudia historia inayotuonesha kwamba wanachuoni wa Kisahaba walikuwa wakimuuliza Ali kwa kila lililowatatiza, na kauli ya Umar bin Al-Khatab aliyoisema zaidi ya mara sabini ya kwamba "Lau kama si Ali basi Umar angeliangamia' لولا علي لهلك عمر wakati ambapo Imam Ali (a.s.) hakupata kamwe kumuuliza Sahaba yeyote miongoni mwao.

Kama ambavyo historia inakiri kuwa Ali bin Abi Talib ni shujaa mno na mwenye nguvu kuliko Masahaba wote, na kuna mashujaa wengi miongoni mwa Masahaba waliokimbia vita katika sehemu nyingi tu, wakati ambapo Imam Ali (a.s.) alisimama imara mahala pote palipopiganwa vita, na inatosha kuwa ni dalili ile nishani aliyopewa na Mwenyezi Mungu pale Mtume (s.a.w.w) aliposema:

"Kesho nitampa bendera yangu mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, naye anapendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, mkali katika mapambano si mwenye kukimbia, Mwenyezi Mungu amekwisha unawirisha moyo wake kwa imani".

Masahaba wakaitamania (kuipata) bendera hiyo, Mtume akampa Ali bin Abi Talib.

Kwa kifupi, bila ya shaka maudhui ya elimu , nguvu na ushujaa, ni sifa ambazo Imam Ali alikuwa nazo, ni maudhui yanayofahamika kwa wote (Sunni na Shia) na ukiachilia mbali maandiko yanayojulisha kwa uwazi wa kuashiria juu ya Uimamu wa Ali, hapana shaka kwamba Qur'an haikubali uongozi na Uimamu isipokuwa kwa mtu mwenye elimu, shujaa tena mwenye nguvu.

Mwenyezi Mungu anasema kuhusu wajibu wa kuwafuata wanachuoni (wenye elimu). pale Allah (s.w) aliposema:-1 2 3 4 5 next