NJIA SAHIHIDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU KUTAMBULIWA NJIA SAHIHI KUPITIA MSINGI WA DINI YA HAKI Hatua ya kwanza: Umuhimu wa maudhui (mada). 1. Kila haki imebeba maumbile mawili, umbile la ndani na umbile la nje, maumbile hayo huthibitishwa na kusadikishwa kutokana na ukweli wa haki hiyo, kwa ufafanuzi zaidi tunaweza kusema hivi:- Haki ni Madhumuni ya ufafanuzi huo tunakusudia kusema hivi:- Dini nayo ni mfano wa kombe na lulu hiyo, - kadiri ya umbile la nje la dini lilivyo na thamani. Basi umbile la ndani la dini pia lina thamani- umbile la ndani la dini limebeba elimu na hukumu za mambo tofauti ya dini, umbile hilo haliwezi kusadikishwa au kuthibitishwa bila ya kuwepo umbile la nje la dini, umbile ambalo linaonyesha msingi wa dini, tukizingatia kuwa umbile la nje la dini ni lazima liwiane na umbile la ndani la dini, kwa hiyo ili kuifahamu dini (ambayo ni umbile la nje) ni lazima tuelewe umuhimu wa elimu na hukumu zote (ambazo ni umbile la ndani) - moja baada ya nyengine - zilizomo katika dini. Kutokana na maelezo hayo, tumefahamu kuwa ni lazima kuelewa umuhimu na falsafa ya dini, na tunaweza kufahamu falsafa hiyo kwa kuzingatia umbile la ndani na la nje la dini.
|