UTUKUFU WA QURANDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU UTUKUFU WA QUR_ANI TAKATIFU Sifa za Sura Al-Hamd (Al-Fatihah) Miongoni mwa Sura za Qur’ani Tukufu, Sura hii inayo hadhi ya juu, ambayo hunyanyuka kutoka kwenye sifa zifuatazo: 1. Uzito wa Sura hii: Kimsingi, sura hii inayo tofauti iliyo wazi na sura zingine za Qur’ani Tukufu kutokana na mtazamo wa uthabiti na uzito, kwa sababu sura zingine zote zinatoka kwenye usemi wa Mungu ambapo Sura hii inatoka kwenye ulimi wa waja. Na kutoka kwenye Mtazamo mwingine katika Sura hii, Mungu amewafundisha waja wake namna ya kusema na kuwasiliana na Yeye” Utangulizi wa Sura hii umeanza na kumsifu na kumtukuza Mola Mlezi. Inaendelea na imani mwanzoni na baada ya maisha ya hapa duniani (kumtambua Mungu na imani katika ufufuo), inaisha na mahitaji na masharti ya waja.
|