WATOTO NI NEEMA
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

WATOTO NI NEEMA YA WAZAZI KUTOKA KWAKE MOLA MTAKATIFU

Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:-

Qur’ani imetaja ya kwamba, mwanadamu ameumbwa kutokana na tone la manii lililochanganyika:

إِنَّا خَلَقْنَا الإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ اَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعاً بَصِيراً[1]

Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.

Hii inaonyesha kwamba, mtoto azaliwaye na wazazi ambao si ndugu wa karibu atakuwa na uwerevu, utambuzi na mwenye nguvu za kimwili kuliko mtoto aliyezaliwa na wazazi wenye uhusiano wa karibu. Hii inaweza kuonekana kwamba Uislamu umezitangulia (kwa uvumbuzi) kanuni za kisayansi na elimu ya ‘tabia zinazorithishwa’ (Heredity) kwa kuonyesha umuhimu ulioko katika sehemu ya urithi wa tabia, na namna gani uteuzi mzuri wa watu wawili wanaooana utakavyopelekea kupata watoto ambao ni tuzo la Mwenyezi Mungu na furaha ya maisha.

Kwa kuwa mtoto atachukua mwenendo wa wajomba na shangazi zake, asili ya undani ya baba yake na mama yake, na akajifunza kupitia kwa urathi ambao umepitia kutokana kwa muungano wa baba yake na mama yake, na ndipo Uislamu ukazitengeneza asili hizi kwa njia hiyo ili kumhifadhi mtoto awe ni kiumbe mwenye heshima na nidhamu, na hivyo kuepukana na upungufu wowote. Mara tu mtu anapoanza kufikiria kuoa na kutunza familia, Uislamu unamuongoza kupitia katika njia hizo.

3. Familia katika Uislamu Familia katika Uislamu, ina utaratibu mzuri na wa hali ya juu sana, na ni utaratibu unaoheshimiwa sana hata ina mahali panapostahiwa. Ni kwa sababu hii na ndio maana Uislamu huipa nguvu (familia) kuanzia mwanzo wa nguvu yake. Ndoa ni sura mpya katika njia ya kuunda jamii, na uangalifu wa Uislamu katika nguzo hiyo muhimu, hatimaye unaongoza kuelekea katika maisha ya amani na furaha.

4. Pendo la wazazi Mtoto ni matokeo ya kimaumbile ya uhusiano imara wa wazazi, ubaba na umama ni matamko mawili ambayo Mwenyezi Mungu ameyazatiti kwa ihsani na mapenzi Yake, akayatajirisha na kuyapitia kwa maana ya kuungana watu wawili na kuendelea kuwa pamoja. Uhusiano wa karibu zaidi baina ya wazazi na watoto wao, ni miongoni mwa uhusiano ulio imara na wenye daraja ya juu zaidi kuliko uhusiano wowote ule wa kibinaadamu. Uhusiano huo umehifadhiwa na Mwenyezi Mungu, naye amehakikisha kuwa unaendelea na kustawi; kwa sababu kufanya hivyo ni kuendelea kwa jamii ya binaadamu na uhai. Upendo wa wazazi kwa watoto wao hauna nafasi yoyote ya kutia shaka, kwani ni alama ya Mwenyezi Mungu na ni neema Yake kubwa kwa walimwengu. Mwenyezi Mungu amesema: “Na katika alama zake, ni huku kuwaumbia wake zenu, kutoka miongoni mwenu ili mpate utulivu kwao, na akajaalia mapenzi na huruma baina yenu.” (30:21). Baadhi ya wafasiri wameeleza ‘penzi’ na ‘huruma’ hapa, kwa maana ya mtoto ambaye ameupa nguvu uhusiano baina ya wazazi na ameupa amani na usalama.1 2 3 next