HAKI ZA WATU KATIKA JAMIIDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU HAKI ZA WATU KATIKA JAMII Mwenyeezi Mungu Mtukufu amempa mwanaadamu hadhi na heshima kubwa kulinganisha na viumbe wengine. Mwanaadamu ana haki na mahitajio mbali mbali katika jamii, kama vile chakula, kivazi pamoja na makazi, ni rahisi kuweza kumtekelezea mnyama Si jambo gumu sana kwa serikali kuweza kuitimizia jamii mahitajio ya kimwili kwa usawa bila ya kubagua, lakini ni vigumu serikali hiyo kuweza kuyatekeleza mahitajio ya jamii ya kiroho, hii ni kwa kutokana na kua kila mmoja ana maradhi maalum yanayoisumbua roho yake na mara nyingi maradhi hayo hutofautiana kwa jinsi ya watu walivo. Moja kati ya mambo yenye kuifanya jamii iridhike na serikali Sote tunaelewa kua katika karne zilizopita Ukiristo ulikua umshika hatamu katika nyanja tofauti za kidini na kidunia, lakini kwa kutokana na matendo ya Kanisa yalivyokua si yenye kuziridhisha nyoyo za watu pamoja na kushindwa kwa Kanisa katika kuyatimiza mahitajio ya jamii, jambo ambalo limesababisha jamii ya kimagharibi kuhisi kua dini haina uwezo wa kuyatimiza mahitajio ya wanaadamu, na linaloonekana hivi sasa katika jamii ni kuikimbia dini na kuivamia dunia kwa kutapatapa huku wakidhani kua matamanio yao ndiyo yawezayo kuiongoza nafsi ya mwanaadamu.
|