TAREHE YA KIISLAMU 02
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMMILAHI RAHMANI RAHIYMI

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ndoa ya Fatima Zahra na Ali ibn Abi Talib

Allah (s.w) aliwapa ushindi Waislamu katika vita vya badr katika mwaka wa 2 wa Hijiria. Miezi miwili baada ya vita hivyo, Fatima Zahra, binti yake Muhammad Mustafa, na Ali, mwana wa Abi Talib walifunga ndoa.

Fatima Zahra alikuwa na miaka mitano tu wakati mama yake - Khadija (R.a.), alipofariki, na kuanzia hapo na kuendelea, baba yake, Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alichukua wajibu wa kazi za mama pia kwa ajili yake. Kifo cha mama yake kilileta pengo katika maisha yake lakini baba yake alilijaza kwa upendo na huruma.

Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliweka uangalifu wa hali ya juu kwenye elimu na malezi ya binti yake. Kama alikuwa ndiye mfano bora kwa watu wote, binti yake alikuwa awe mfano bora kwa wanawake wote, na alikuwa hivyo. Alimfanya yeye kuwa mfano bora wa uwanauke katika Uislamu. Alikuwa ni mfano halisi wa ibada na utii kwa Muumba, na alikuwa ni mfano halisi wa usafi wa ki-ungu na utakatifu. Katika tabia na hulka, alikuwa na mfano unaovutia sana kwa baba yake. Fatima, binti huyu, alikuwa ni picha ya Muhammad, baba yake.

Kwa kufanya utii na ibada kwa Allah (s.w.t.) Fatima Zahra alipanda kufikia cheo kikubwa mbele ya Allah (s.w.t.) kama ilivyoshuhudiwa na Qur'an Tukufu. Allah (s.w.t.) alimpa utukufu mkubwa sana juu yake, na Mtume wa Uislamu (s.a.w.), kwa upande wake, alim-wonyesha kiwango cha heshima ya juu sana, moja ambayo hakuionyesha kwa mwanaume au mwanamke mwingine yeyote yule katika wakati wowote wa maisha yake.

Wakati Fatima alipokuwa, maswahaba wawili wazee - wa kwanza na kisha baadae mwingine - walimuomba baba yake wamchumbie. Lakini aligeukia pembeni kwa kuchukia, na akasema:

"Hili suala la ndoa ya Fatima, binti yangu, liko mikononi mwa Allah (s.w.t.) Mwenyewe, na Yeye pekee ndiye atamchagulia yeye mchumba".

Allah (s.w.t.) alifanya uchaguzi Wake kama ipasavyo. Alimchagua mja Wake, Ali ibn Abi Talib, kuwa ndiye mchumba wa binti ya mja Wake mpendwa mno, Muhammad Mustafa. Alipenda kuwaona Fatima binti Muhammad na Ali ibn Abi Talib wakioana.1 2 3 next