Ali vitani
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

IMAMU ALI (A.S) KATIKA VITA VYA KIISLAMU

Waislamu na Wayahudi

Mnamo mwaka wa 70 A.D. Yule jenerali wa Kirumi, Titus, aliiteka Jerusalem na akakome-sha utawala wa Kiyahudi wa Palestina. Kufuatia utekaji nyara wa Warumi, Wayahudi wengi waliondoka kwenye nchi yao na wakatangatanga kwenye nchi nyingine. Baadhi ya makabila ya Kiyahudi yalivuka jangwa la Syria na kuingia kwenye peninsula ya Arabia ambako waliweka makazi yao huko Hijazi. Baada ya kupita muda walijenga makoloni mengi huko Madina na kati ya Madina na Syria. Wanasemekana pia kwamba waliwabadili Waarabu wengi na kuwaingiza kwenye Ujuda (dini ya Wayahudi).

Mwanzoni mwa karne ya saba A.D., kulikuwa na makabila matatu ya Kiyahudi yaliyokuwa yanaishi Madina (Yathrib). Haya yalikuwa ni Banu Qainuka'a, Banu Nadhir na Banu Qurayza. Makabila yote matatu yalikuwa matajiri na yenye nguvu, na pia, yalikuwa yamestaarabika zaidi kuliko hao Waarabu. Wakati ambapo Waarabu walikuwa wote ni wakulima, hawa Wayahudi walikuwa wawekezaji mali wa viwanda, biashara na uchuuzi katika Arabia, na walisimamia maisha ya kiuchumi ya Madina (Yathrib). Yale makabila mawili ya Kiarabu - Aus na Khazraj - walikuwa wamejawa na madeni kwa Wayahudi daima.

Mbali na Madina, vituo vizito vya Wayahudi katika Hijazi vilikuwa Khaibar, Fadak na Wadi-ul-Qura. Ardhi katika mabonde haya ilikuwa ndio yenye rutuba zaidi katika Arabia yote, na wakulima wake wa Kiyahudi walikuwa ndio wakulima wazuri zaidi katika nchi hiyo.

Kule kuhama kwa Muhammad, Mtume wa Uislamu, kutoka Makka kwenda Madina (wakati huo Yathrib) kulimkutanisha na Wayahudi kwa mara ya kwanza. Hapo mwanzoni walikuwa na urafiki naye. Aliwapa ule mkataba maarufu wa Madina, na wakamtambua yeye kama mtawala wa mji wao, na wakakubali kufuata uamuzi wake katika migogoro yote. Walikubali pia kuulinda mji huo katika kitendo cha kuvamiwa na adui.

Lakini, kwa bahati mbaya, urafiki huu haukudumu kwa muda mrefu. Mara moja ikaonekana wazi kwamba hao Wayahudi walitoa urafiki wao kwa Muhammad kwa masha-ka mengi. Kwa maslahi yao binafsi, walipaswa kutekeleza wajibu wao wa makubaliano kwa uaminifu lakini hawakufanya hivyo. Kwa mabadiliko haya katika tabia zao, kulikuwa na sababu nyingi, miongoni mwao zikiwa:1 2 3 4 5 next