MRITHI WAKE BAADA YA YEYE KUFARIKI?Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU HISTORIA YA KIISLAMU HIVI KWELI HADHARATI MUHAMMAD (S.A.W.W) ALIMTEUWA MRITHI WAKE BAADA YA YEYE KUFARIKI? Haiwezi kupingika kwamba Mustashriq wengi wametoa michango isiyofaa kabisa kwenye uchunguzi, elimu na ufahamu wa Uislamu. Ni kutokana tu na jitihada zao kwamba hazina nyingi zisizo na thamani, za historia, fani na fasihi za Kiislamu zimeokolewa kutokana na kusahaulika, na zimekuwa zimehifadhiwa. Inawezekana kabisa kwamba hazina nyingi kama hizo zingeweza kupotea daima Lakini licha ya mapenzi na hamu ya elimu, na kujifunga kwenye ukweli kwa wanafunzi wa Magharibi, inaonekana kwamba wakati wengi wao wanapoufafanua Uislamu, historia yake na sheria zake, jambo fulani huenda kombo. Ni vigumu kuamini lakini ni kweli kwamba baadhi Nimenukuu hapo juu utaratibu wa kuandika historia ya kisa yansi na isiyo na upendeleo kama ulivyoelezwa Mfano wa dhahiri wa uzuzu huo, na msingi wa kutotambua wa hawa Mustashriq, kuhusu suala hili, ni kule kukubaliwa na wao, kama "ukweli" wa kihistoria wa ile taarifa ya uwon-go kwamba Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) alifariki bila ya kumteua mtu yeyote kama mrithi wake, na kwamba aliliacha suala la kumtafuta kiongozi wa umma wa Waislamu kwenye hiari ya wafuasi wake wenyewe. Hakuna Mustashriq aliyesita na kufikiria, kwa kiasi ninavyotambua mimi, ili kuchunguza kama hili ni kweli au kama ni lenye uwezekano wa kuwa kweli kwamba Muhammad ali-watelekeza Waislamu bila ya kiongozi, na ikawabidi kumpata kiongozi katika mfumo usio na mipaka na unaoruhusu kila mbinu, wa kikatili, huru kwa wote na kushindana kwa ajili ya madaraka. Ili kuepukana na kazi ngumu ya kutafuta ukweli, Mustashriq wamekubaliana tu na wanahistoria wa Sunni kwamba Muhammad, Mtume wa Uislamu, hakuwa na chaguo au upendeleo katika suala la urithi wake mwenyewe; na lolote lililotokea ndani ya Saqifah kwa hiyo, lilikuwa ni sawa na halali, na pia lilikuwa kwa faida kubwa ya umma wa Waislamu.
|