KUTEKWA KWA MAKKA
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kutekwa kwa Makka

Maquraishi walishindwa kutumia ushindi wao wenyewe juu ya Waislamu katika vita vya Uhud, lakini hawa Waislamu waliposhindwa katika vita vya Muutah na Wakristo, wali-jaribu kutumia ule ushindi wa Wakristo, na kurudisha ile hali ya kabla y a Hudaybiyya katika Arabia. Kushindwa kwa Waislamu kule Muutah kulichukua nafasi kubwa katika matukio yaliyotangulia kuanguka kwa Makka mnamo mwaka 630.

Tunaweza kukumbuka kwamba mara tu Khalid na lile jeshi waliporudi Madina bila ya uthibitisho wa ushindi (katika vita vya Muutah), waliitwa wakimbizi. Askari wengi na makamanda walijihisi kuabika sana kiasi kwamba walikaa majumbani ili wasionekane na kudhalilishwa hadharani. Vile vita vya Muutah viliwapa Maquraishi ile picha kwamba Waislamu na nguvu zao sasa wameangamizwa na kwamba, hadhi yao na hofu ambavyo hapo kabla waliviingiza kwa wengine vyote vimetoweka. Hii iliwafanya Maquraishi kuegemea kwa nguvu sana kwenye hali zilivyokuwepo kabla ya Mkataba wa Hudaybiyya. Walidhani sasa wangeweza kuanzisha vita ambavyo dhidi yake Waislamu walikuwa hawawezi kujihami wenyewe, bila kuzungumzia juu ya kujibu mashambulizi au kulipiza kisasi.

Kulingana na makubaliano ya ule Mkataba wa Hudaybiyya, yale makabila ya Waarabu yalikuwa huru kuingia kwenye mahusiano ya mkataba ama na Waislamu au hao Maquraishi. Kwa kuchukua fursa ya mapatano haya, lile kabila la Banu Khuza'a waliandi-ka mkataba wa urafiki na Mtume wa Uislamu, na kabila lingine - Banu Bakr - wakawa washirika wa Maquraishi. Uhasama ulidumu baina ya haya makabila mawili tangu nyakati za kabla ya Uislamu lakini sasa yote yalipaswa yafuate masharti ya ule Mkataba wa Hudaybiyya, na kuepuka kushambuliana.

Lakini miezi kumi na nane baada ya huo Mkataba wa Hudaybiyya kutiwa saini, kundi la wapiganaji la Banu Bakr ghafla likawashambulia Banu Khuza'a majumbani mwao wakati wa usiku. Wakati wa shambulio hili unatolewa kama ni mwishoni mwa Rajab ya mwaka wa 8 A.H. (Novemba 629). Banu Khuza'a hawakufanya chochote kuchochea shambulio hili. Walichukua hifadhi katika maeneo ya Al-Kaaba lakini maadui zao waliwafuatilia hata hapo, na wakawaua baadhi yao. Wengine waliokoa maisha yao kwa kutafuta ulinzi wa Budail bin Waraka na rafiki yake, Rafa'a, katika nyumba zao, hapo Makka.

Ule Mkataba wa Hudaybiyya uliandika kwamba mtu yoyote asiye wa Makka akitaka kujiunga na kambi ya Muhammad au ile ya Maquraishi anaweza kufanya hivyo bila ya kipingamizi. Kwa msingi wa kipengele hiki, lile kabila la Khuza'a lilijiunga na safu ya Muhammad, na lile la Banu Bakr likajiunga na Maquraishi. Kati ya Banu Khuza'a na Banu Bakr idadi ya migogoro ya zamani ambayo ilikuwa haijasuluhishwa ilibidi isimamishwe kwa sababu ya mipango mipya. Pamoja na Maquraishi kuamini kwamba (baada ya vita vya Muutah) uwezo wa Waislamu umevunjika, Banu al Dil, ukoo mmoja wa Banu Bakr, walidhani kwamba muda umefika wa kilipiza kisasi chao dhidi ya Khuza'a.

Banu Bakr wasingeweza kuwashambulia Khuza'a bila ya kula njama na kutiwa moyo kama sio kuungwa mkono kwa uwazi na Maquraishi. Tabari, yule mwanahistoria, anase-ma kwamba Ikrima bin Abu Jahl, Safwan bin Umayya na Suhayl bin Amr, wote watu mashuhuri wa Quraishi, walijibadili wenyewe na kupigana kwenye upande wa Banu Bakr dhidi ya Khuza'a. Kati ya hawa watatu, huyu wa mwisho kutajwa ndiye mweka saini mkuu wa Maquraishi kwenye Mkataba wa Hudaybiyya.

Katika Rajabu ya mwaka wa 8 (Novemba 629), katika mfululizo wa kisasi cha kurithi baina ya koo ambacho kilikuwa kikiendelea kwa miongo kadhaa, baadhi ya wale waliotaharuki sana katika Maquraishi kule nyuma yao, walishambulia kikundi cha kabila la Khuza'a, washirika wa Muhammad, sio mbali sana kutoka Makka. Mtu mmoja aliuawa na waliobakia waliumizwa vibaya na kulazimishwa kukimbilia ndani ya eneo tukufu la Makka. Wakifuatiliwa hata huko walichukua hifadhi kwenye nyumba mbili za kirafiki. Kwa aibu sana hawa Banu Bakr waliweka mzingiro kwenye nyumba hizo. Kwa jumla watu ishirini wa Khuza'a waliuliwa.

Mmoja wa wakuu wa Khuza'a, Amr bin Salim, alikwenda Madina na kumsihi Mtume (s.a.w.w) kuingilia kati. Mtume alishituka kusikia habari hizo za ufisadi. Kama mshirika wa hao Khuza'a, alipaswa kuwalinda kutokana na maadui zao. Lakini kabla ya kufikiria hatua za kijeshi, alijaribu kutumia njia za amani ili kupata marekebisho na haki. Alituma mjumbe kwa Maquraishi, na akashauri kwamba:1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 next