MAISHA YA MTUMEDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI WALAHALA WALA KUWATA ILLA BILAHI AL_ALIYYU AL_ADHIM MAISHA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) Umrah au Hijja Ndogo - A.D.629 (8 H.A.) Mwaka mmoja baada ya Mkataba wa Hudaybiyyah, Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.w) alikwenda Makka kufanya hijja. Alifuatana na Waislamu elfu mbili. Kulingana na mashar-ti ya Mkataba huo, wale washirikina waliihama Makka kwa siku tatu. Waislamu waliuin-gia mji kutokea upande wa kaskazini, na hawakuwahi kumuona mtu yoyote wa Makka. Mtume wa Allah (s.a.w.w) alimpanda ngamia-jike wake, al-Qas 'wa. Rafiki yake, Abdullah ibn Rawaha, alishikilia hatamu zake alipokuwa akiingia maeneo ya Al-Kaaba. Alikuwa anasoma Aya za ile Sura inayoitwa, Ushindi, kutoka kwenye Qur'an. Waislamu wengine walikuwa wakiitikia kwa kurudia "Tuko chini ya amri Yako, Ewe Allah (s.w.t.)! Tuko chini ya amri Yako, Ewe Allah (s.w.t.)! Wakati Waislamu wote walipokuwa wamekusanyika ndani ya uwanja wa Al-Kaaba, Bilal alipanda juu ya jengo Washirikina walikuwa wakishuhudia mandhari hii kutoka kwenye vilele vya vilima vinavyozunguka lile bonde la Makka. Hawajawahi kuona nidhamu ya namna hiyo hapo kabla, wakati Waislamu wa uzao-bora walipokuwa wakitii bila ukaidi, wito wa mtumwa wa zamani wala hawajaona udhihirisho wa usawa na umoja. Lile kundi kubwa la Waislamu lilisogea kama mwili mmoja, na Maquraishi waliweza kuona kwa macho yao wenyewe kwamba ulikuwa ni mwili ambamo mlikuwa hamna utofautishaji kati ya matajiri na masikini, mabwana na watwana, weusi na weupe, na Waarabu na wasiokuwa Waarabu. Maquraishi pia waliweza kuona kwamba ule udugu, usawa na umoja wa watu ambao Uislamu ulikuwa unauendeleza haukuwa dhana ya kinadharia bali ulikuwa ni kweli tupu. Ilikuwa ni mandhari ya kuvutia Ule mwenendo wa Waislamu ulikuwa wa namna yake. Walikuwa na shauku Na bado udhihirishaji huu ndani ya Al-Kaaba wa nidhamu wa Waislamu, ulikuwa usio-fanyiwa mazoezi, uliojitokeza wenyewe kabisa. Si kwa chochote katika dunia hii ambacho Mwarabu alikuwa na mzio (allergic)
|