TAREHE YA KIISLAMU
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI


WALA HAWLA WALA KUWATA ILA BILAHI

 

AL_ALIYYU AL_ADHIYM

 

HISTORIA YA KIISLAMU

 

Waislamu wasusiwa kiuchumi.

Kususiwa kiuchumi na kijamii kwa Bani Hashim

Mwaka wa sita wa Tangazo ulikuwa unakaribia. Wapagani walikuwa tayari wamemaliza miaka mitatu kupiga kampeni dhidi ya Uislamu. Wamezalisha uchungu mwingi na uhasama dhidi ya Waislamu katika miaka hii mitatu, lakini walikuwa na kidogo sana, kama kilikuwapo chochote, cha kuonyesha kwa ajili ya juhudi zao. Walitumia kila silaha dhidi ya Waislamu kuanzia vivutio mpaka ushawishi, hadi matusi mpaka kebehi, na dhihaka mpaka vitisho vya kutumia nguvu na utumiaji hasa wa nguvu zenyewe, lakini bila mafanikio. Ile nguvu ya imani ya Waislamu iliwakanganya.1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next