UANDISHI WA BARUA YA MTUME (S.A.W.W)
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KISA CHA UANDISHI WA BARUA (WASIA WA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)

Ufafanuzi wa kisa hicho ni kama ifuatavyo:

(Pindi Mtume alipofikiwa na kipindi cha kuiaga dunia (kukata roho) –Ihtidhaar- na nyumbani kwake kukiwa na watu kadhaa miongoni mwao akiwemo Omar bini- Khattab, Mtume (s.a.w.w) alisema: Nileteeni kalamu na karatasi nikuandikieni mambo ambayo pindi mkiyazingatia na kuyafanyia amali hamtopotea kamwe baada yangu, Omar akasema: Hakika Mtume amezidiwa na maumivu (anaweweseka), nasi tunacho kitabu cha Mwenyezi Mungu (Qur'an), kinatutosha, watu waliokuwa nyumbani kwa Mtume wakahitilafiana na kugombana pia kupigishana kelele, kati yao kukiwa na wale wasemao: Mpeni kalamu na karatasi ili Mtume akuandikieni mambo ambayo hamtopotea kamwe baada yake, na kati yao wamo waliokuwa wakisema kama yale aliyo yasema Omar, na pindi walipozidisha kelele natofauti mbele ya Mtume (s.a.w.w) Mtume  wa Mwenyezi Mungu akawambia: Tokeni nje. Na Ibnu Abass baada ya tukio hilo akisema:

(Hakika huzuni iliyokuwa kubwa zaidi ni kule kumzuilia Mtume wa Mwenyezi Mugu kupewa karatasi ili awaandikie usia ule kutokana na tofauti yao au kutofautiana kwao na kugombana kwao)[1] .

Sayyid Sharafud-din amesema akielezea juu ya tukio hilo:

(Na hadithi hii ni hadithi ambayo hakuna tofauti juu ya usahihi wake wala juu ya kutoka kwake kwa Mtume, na kwa hakika bwana Bukhari ameipokea hadithi hiyo katika sehemu nyingi katika sahihi yake, na imetolewa na Muslim mwishoni mwa usia katika sahihi yake pia, na imepokelwa na Ahmad  kati ya hadithi za Ibnu Abbas katika Musnadi wake, na waandishi wengine wa vitabu vya Sunan na vitabu vya hadithi).[2]

( Na tukizingatia katika kauli yake Mtume (s.a.w.w) isemayo:

(هلم اكتب لكم كتاباً لن تضلوا بعده)

(Leteni kalamu na karatasi nikuandikieni mambo ambayo hamtopotea baada yake) na kauli yake iliyoko kwenye hadithi ya vizito viwili (Thaqalain) isemayo:1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 next