UIMAMUDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI UIMAMU Uimamu: kwa maana ya kilugha ni masdari (chimbuko) kwa kipimo cha .( فِعالة ) ambalo ni mudha'afu, na husemwa: (أَمَّ القوم وبالقوم يؤُمهم أَمَّاً وإماماً وإمامة، مثل : كتب يكتب كَتْبا ً وكِتابا ً وكتابة.) Na jina la mtendaji litokanalo na kitendo ( أم - يؤم) ni آم asili yake ni (أصله آمم ) kisha mim moja ikaunganishwa na mim nyingine (ikafanyika idghamu). Lakini hutumika sana masdari ya kitendo hicho kwa maana ya jina la mtendaji, kwa hivyo husemwa: Imam kwa swigha ya kiume na kike kwa ajili ya mwanamume na mwanamke, na wingi wake ni (أيمة) kwa (yee), na ( أئمة ) kwa Hamzah. Na maana yake-kutokana na kamusi-ni uongozi au mtu anaefuatwa kauli zake na matendo yake, sawa awe kwenye haki au batili. Na neno hilo limetumika ndani ya Qur'an tukufu kwa Imam wa haki au mwenye kuongoza kwenye haki kama kauli hii ya Allah isemavyo: وجعلناهم أئمة يهدون بأمرنا)[1])
|