DALILI ZA UKHALIFA ZA AHLI SUNNADeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI DALILI ZA AHLI-SUNNA JUU YA UIMAMU WA ABUBAKAR SIDIQ: 1-DALILI YA WAZI: Ahli sunna ambao wanaamini kuwa Mtume alitoa dalili ya wazi juu ya Abubakar walishikamana na hadithi mashuhuri kuthibitisha madai hayo nayo ni (Hakika mwanamke mmoja alikuja kwa Mtume (s.a.a.w) kumuuliza jambo moja wapo katika ya mambo aliyotaka kumuuliza na mtume kumjibu na kumtaka arejee kwake wakati wowote atakapo taka, yule mama akasema: Unaonaje nikija na nisikukute? Mtu akasema: Ikiwa hukunikuta basi mwendee Abubakar). Na katika hadithi nyingine imepokelewa kuwa: (اقتدوا باللذين من بعدي : ابي بكر وعمر) (Wafuateni wale wajao baada yangu: Abubaka na Omar). Na katika hadithi ya Abi hurairah amesema: (Amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akisema: “Nilipokuwa nimelala nilijiona na kujikuta nikiwa juu ya kisima na juu yake kukiwa na ndoo, nikachota humo kiwango alichokitaka Mwenyezi Mungu, kisha akaichukua ndoo hiyo mtoto wa Abi Quhafah akatoa na kuchomoa humo dhambi moja au madhambi mawili, na katika utoaji wake alikuwa dhaifu, na Mwenyezi Mungu amsamehe udhaifu wake, kisha ikageukia upande wa magharibi, akaichukua Omar mtoto wa Al-khattab, sikumuona mtu mwenye akili ya kiwango cha juu zaidi kati ya watu aliekuwa akitoa nakuchomoa kama utoaji wa Omar mpaka akawapiga watu…”.
|