ALI NA VITA VYA TABUK
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

IMAMU ALI BIN ABI TALIB NA VITA VYA TABUK

VITA VYA TABUK

Vita vya Muutah ambavyo Waislamu walishindwa, vilipiganwa mnamo Septemba mwaka 629. Kushindwa kwao kulitafsiriwa katika jamii nyingi kama ni ishara ya kuanguka katika mamlaka ya Dola mpya ya Kiislamu. Maharamia wa Kiarabu lazima watakuwa wame-ona inatia hamu kushambulia Madina baada ya kuanguka huku kwa kubuniwa. Lakini katika kiangazi cha mwaka 630, minong'ono ilikuwa ikizunguka hapo Madina kwamba hayakuwa yale makabila ya Arabia ya kaskazini bali ni vikosi vya Kirumi ambavyo vilikuwa vinajikusanya katika mpaka wa Syria kwa ajili ya uvamizi wa Hijazi.

Muhammad, Mtume (s.a.w.w) wa Uislalmu, aliamua kuchukua hatua za tahadhari kwa ajili ya ulinzi wa Madina, na akawaamuru wafuasi wake kujiandaa na mapambano marefu upande wa kaskazini.

Ilikuwa ni mwezi wa Septemba, na hali ya hewa ya Hijazi mwaka ule ilikuwa ni ya joto kupita kiasi. Zaidi ya hayo, ukame mrefu ulitishia jimbo hilo na hali ya nusu njaa. Majibu ya Waislamu, kwa hiyo, yalikuwa yamepooza sana. Hawakupenda kuondoka majumbani mwao kwa wakati kama huu.

Mnamo Septemba au Oktoba 630, Mtume wa Allah (s.a.w.w) alitoa amri ya kujiandaa kwa msafara wa kwenye mpaka wa Byzantium. Hali ya hewa ya Hijazi ilikuwa bado ni ya joto kali sana, maji na malisho yalikuwa adimu, na mizunguko ya jeshi kubwa kama hilo ingekuwa ni migumu sana. Huenda kumbukumbu za maafa ya Muutah zili-wakosesha watu wengi nia ya kupambana na Byzantium tena.

Washirikina hapo Madina waliichukua fursa hii kupandikiza mfarakano katika vichwa vya waumini wapya katika Uislamu. Sio kwamba hawakushiriki tu katika vita bali pia wali-jaribu kuwageuza wengine mawazo kutofanya hivyo. Katika jaribio la kudhoofisha nia na makusudi ya Waislamu, walianza kueneza habari za wavumishaji wa mambo ya kutisha kwamba maadui safari hii hawakuwa wale askari wa kikabila wa kuchukuliwa kwa nguvu, masikini, wenye zana duni, wasiojiamini na wajinga waliopigana bila mpango na bila nid-hamu bali ni Warumi ambao walikuwa ndio dola iliyoendelea sana na yenye nguvu sana duniani, na ambao, kwa kweli, watawateketeza Waislamu.

Hata hivyo, Waislamu wengi waliitika kwenye mwito wa Mtume, na wakachukua silaha kuilinda dini. Wakati ilipochukuliwa idadi ya vichwa, walipatikana watu 30,000 walioji-tolea. Lilikuwa ndio jeshi kubwa sana lililowahi kukusanywa katika Arabia hadi hapo.

Mtume (s.a.w.w) alimteua Ali ibn Abi Talib kama kaimu wake hapo Madina wakati wa kutokuwepo kwake yeye mwenyewe. Alimchagua Ali kuwa kaimu wake kwa sababu zifu-atazo:1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 next