ALI AMHAMI MTUME (S.A.W.W)Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI IMAMU ALI (A.S) AMUHAMI MTUME (S.A.W.W) NA KUULIWA NA MAKUREISHI Usahihi wa Historia ya Uislamu kuhusiana na Imamu Ali (a.s) na Waislamu Wakati Waislamu wengi walipoondoka Makkah na kufanya makazi huko Yathrib, ilionekana kwa waabudu masanamu kwamba kama Uislamu utapata mizizi katika ile Nchi ya CHEMCHEM iliyopo kaskzini mwao, na ukaweza kujitegemea, itakujaleta tishio kwenye maslahi Mtume, hata hivyo, alikuwa tayari kukutana na dharura Muhammad Husein Haykal. Wale vijana ambao Maquraishi waliwaandaa kwa ajili ya kutekeleza mauaji ya Muhammad walikuwa wamezingira (wameizunguka) nyumba yake wakati wa usiku ili asije akatoro-ka. Katika huo usiku wa Hajira, Muhammad alitoa siri ya mpango wake kwa Ali ibn Abi Talib na akamuomba ajifunike shuka la kijani la Mtume, na alale kwenye kitanda cha Mtume. Alimuomba tena akae hapo Makka mpaka atakapokuwa amerudisha vitu vyote vya thamani vilivyokuwa vimewekwa kwa Muhammad, kwa wenyewe. "Wauaji walikuwa mbele ya nyumba yake (Muhammad). Alitoa shuka lake kwa Ali, akimtaka alale kwenye kitanda hicho ili kwamba yeyote atakayekuwa anatazama ndani angefikiria kwamba Muhammad amelala pale. Washirikina waliizunguka nyumba ya Muhammad. Walichungulia ndani wakaona mtu aliyelala amefunikwa na blanketi, na wakaridhika kwamba "windo" lao liko salama. Ule wasaa wa fursa kwa ajili ya Mtume (s.a.w.w) kutoroka ulifika muda baada ya usiku wa man-ane wakati ambapo wale askari wa doria wamesinzia. Alitembea kimya kimya na kuwapi-ta na kutoka nje ya maeneo ya nyumba yake. Wale askari wa doria wa kipagani walikutwa wamejisahau, na Mtume wa Allah (s.w.t.) ali-fanikiwa katika kuukwepa kwa hila uchunguzi wao!
|