ALI (A.S) AACHWA BILA YA NDUGU
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

ALI (A.S) AACHWA BILA YA NDUGU

Ali ibn Abi Talib pekee ndiye aliyeachwa bila ya "ndugu." Alikuwa anastaajabu kwa nini wakati Mtume wa Allah (s.a.w.) alimshikilia mikononi mwake na akamwambia: "Wewe ni ndugu yangu katika dunia hii na katika akhera."

Muhammad ibn Ishaq:

"Mtume (s.a.w.) mwenyewe alimshika Ali mkononi na kusema: "Huyu ni ndugu yangu." Hivyo Mtume wa Allah (s.a.w.) Bwana wa waliotumwa, na kiongozi wa Wacha-Mungu, Mtume wa Mola wa mbingu na ardhi, asiye na mshirika wala asiyelingana na yoyote, na Ali ibn Abi Talib wakawa ndugu."

"Baada ya safari ya hatari na ya haraka kandoni mwa mwambao wa bahari, Muhammad alisimama hapo Kuba, maili mbili kutoka mjini, na akafanya kuingia kwake kwa uwazi ndani ya Madina siku kumi na sita baada ya kukimbia kwake toka Makka. Wafuasi wake shupavu sana walikusanyika kumzunguka yeye; na walio sawa, ingawa sifa mbali mbali za Waislamu zilitambulikana kwa majina ya Muhajirina na Ansari, wakimbizi wa Makka na wasaidizi wa Madina.

Kufutilia mbali mbegu za wivu, Muhammad kwa hekima na busara akawaunganisha wawili wawili wale wafuasi wake wakuu kwa haki na wajibu wa udugu; ambapo Ali alijikuta binafsi bila mwenza, na Mtume (s.a.w.) kwa upendo mwingi akatamka kwamba yeye atakuwa sahiba na ndugu wa yule kijana mtukufu.

"Wazo la kwanza kumjia yeye (Muhammad) lilikuwa lile la kupanga upya safu za Waislamu ili kuunganisha umoja wao na kufuta kila uwezekano wa kuibuka tena kwa mgawanyiko na uhasama. Kwa kulitambua lengo hili, aliwataka Waislamu kusuhu-biana wao kwa wao kwa ajili ya Allah (s.w.t.) na kujifunga wenyewe wawili wawili. Alieleza jinsi yeye na Ali ibn Abi Talib walivyokuwa ndugu..."

Muhammad, Allah (s.w.t.) ampe rehma na Ahlul-Bait wake, aliwafanya Muhajirina na Ansari kuwa "ndugu" wa kila mmoja wao. Lakini Ali, kama yeye mwenyewe, alikuwa Muhajir (mhamiaji), na bado yeye (Muhammad) alimchagua yeye kuwa ndugu yake. Kwa kufanya hivyo, alikuwa akibainisha kile cheo cha kipekee na hadhi maalum ya Ali katika

Uislamu. Ali, ingawa bado kijana, tayari alikuwa amemzidi kwa cheo kila mtu katika kutu-mikia Uislamu bidii ya wajibu kwa Allah (s.w.t.) na Mtume Wake. Alikipata cheo hiki kikubwa kwa kutumia uwezo wake na tabia.1 2 3 4 5 6 7 8 next