ALIY (A.S) AUZA NAFSI YAKEDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI ALIY (A.S) AUZA NAFSI YAKE KWA KUTAKA RADHI ZA MWENYEEZI MUNGU Allah (s.w) katika ﴿وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِى نَفْسَهُ ابْتِغَاء مَرْضَاتِ اللهِ وَاللّهُ رَؤُوفٌ بِالْعِبَادِ﴾ Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Allah. Allah ni mpole kwa waja wake Razi, yule mfasiri maarufu wa Qur'an, anasema ndani ya Tafsir Kabir yake kwamba Aya hii ilishuka hasa kwa kutambua kazi kubwa na tukufu ya Ali katika usiku wa Hijiria alipomuwezesha Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) kuondoka Makka. Kwa sababu ya Ali, aliweza kuondoka kwa usalama. Katika usiku ule wa kihistoria, ilifanyika shughuli ya kibiashara ya ajabu na ya kimuujiza, ya kwanza na ya mwisho ya aina yake katika historia nzima ya Maumbile. Yalikuwa ni mapatano ya kuuza-na-kununua kati ya Allah (s.w.t.) na mmoja wa waja Wake. Mja aliyehusika hapa ni Ali ibn Abi Talib.[1] Katika usiku mkimya na usio na mbaramwezi, Allah (s.w.t.) alikuja kwenye "soko" Allah (s.w.t.) huyo "Mteja" aliangalia "mfanyabiashara," na bidhaa ikabadilishanwa, sawasawa
|