JEMEDARI AUWAWA
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

BISMILAHI RAHMANI RAHIYM

ALI BIN ABI TALIB (A.S) AMUUWA JEMADARI WA MAKKA

HAMZA AUKUBALI UISLAMU - A.D. 615

Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) ingawa alikuwa yuko salama chini ya ulinzi wa ami yake, Abu Talib, lakini bado hakusalimika na bughudha za washirikina. Wakati wowote walipopata mwanya wa kumuudhi, hawakuupoteza. Wakati mmoja Abu Jahal alimkuta akiwa peke yake, na akatumia lugha ya kishenzi na ya kuchukiza sana juu yake Muhammad. Jioni hiyo hiyo wakati ami yake, Hamza ibn Abdul Muttalib alivyorudi nyumbani kutoka safari ya mawin-doni, mtumwa wake wa kike alimuelezea kile kisa cha fedhuli isiyo na sababu ya Abu Jahal kwa Muhammad na ustahimilifu wa Muhammad, ambao yeye alikuwa shahidi.

Hamza alikuwa mpiganaji, mwindaji na mwanamichezo, na alikuwa hana habari sana na mambo ya kila siku ya mjini hapo. Lakini tabia ya Abu Jahal kwa mpwa wake ilimpan-disha sana hasira kiasi kwamba alichukua upinde wake, na akaingia kwenye mkutano wa Maquraish ambamo yeye Abu Jahal alikuwemo akiwachambulia wenzie matukio ya siku ile.

Hamza akampiga kichwani mwake na upinde wake, na kumsababishia atokwe na damu, na akasema: "Na mimi pia nimekuwa Mwislamu."

Huu ulikuwa ni mtihani kwa Abu Jahal lakini aliona kwamba kimya kilikuwa ni sehemu bora ya ujasiri, na hakugombana na Hamza, pia akawazuia rafiki zake ambao walitaka kusimama kumtetea.

"Ami yake Muhammad, Hamza, mtu wa umri wake mwenyewe, alisifika kuwa mwenye nguvu sana na uwezo kati ya Maquraish, shujaa wao katika vita na michezo. Alitumia muda wake mwingi kwa kuwinda vilimani. Siku moja alipokuwa anarudi kutoka kwenye msako na uta wake ukinin'ginia kwenye bega lake, mtumwa wake wa kike alimweleza jinsi Abu Jahal alivyomrundikia matusi mpwa wake.

Hamza alijikuta mwisho kabisa wa uvumilivu wote. Alimpenda Muhammad, ingawa alikuwa hamuelewi (japo kwa makosa, sio kweli). Alikimbilia Msikitini, ambako alimuona Abu Jahal akiwa amekaa miongoni mwa marafiki zake. Akanyanyua uta wake mzito na akampiga nao pigo kubwa sana kichwani mwake. "Utamtukana tena nitakapojiunga na dini yake?" alipiga kelele, akinyoosha misuli yake mikubwa mbele ya Maquraish.1 2 3 4 5 6 7 next