MASHIRIKIANO YA IMAMU ALIY (A.S)Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI MASHIRIKIANO YA IMAMU ALIY (A.S) KATIKA VITA VYA KIISLAMU Vita ilikuwa ni desturi ya kudumu ya jamii ya kiarabu. Jangwa liliweza kuchukua idadi ndogo tu ya watu, na hali ya vita vya kikabila ilidumisha uthibiti mkali juu ya ongezeko la watu. Lakini Waarabu wenyewe hawakuiona vita katika mwanga huu. Kwao wao, vita vilikuwa burudani au kiasi mchezo wa hatari, au aina ya tamthiliya ya kikabila, iliyofanywa na wenye weledi (ubingwa), kwa mujibu wa mfumo wa kanuni za zamani na ushujaa, ambapo "watazamaji" walishangilia. Amani ya kudumu haikuwa na mvuto kwao na vita vilitoa fursa ya kukwepa kazi ngumu na kutokubadilika kwa mwenendo wa maisha katika jangwa. Wao kwa hiyo walichochea msisimko wa mapambano ya silaha. Vita viliwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika kutupa mishale, ufundi wa kurusha panga na upandaji wa farasi, na pia, katika vita, wangeweza kujipatia sifa kwa ushujaa wao na wakati huohuo kuleta fahari na heshima kwa makabila Anasema G.E.Grunebaum: "Katika karne ya kabla ya kuja Uislamu makabila yalitawanya nguvu zao zote katika vita vya kuviziana, wote dhidi ya wote." Yale makabila ya wahamaji yalizunguka kwenye peninsula yote na kupora misafara na makazi madogomadogo. Misafara mingi na vijiji vilinunua kinga ya mashambulizi Haya kwa kulipa kiwango maalum cha fedha kwa watekanyara wa wahamaji. Ni muhimu kuzingatia ule ukweli katika usiku wa kuzaliwa Uislamu hakukuwa na serikali katika ngazi yoyote katika D.S. Margoliouth: "
|