BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

 

KAULI YA IMAMU ALIY (A.S)KUHUSU BAADHI YA MASAHABA

 

Imam Ali (a.s.) amesema akiwazungumzia Masahaba hawa wanaohesabiwa kuwa ni miongoni mwa (watu) wa mbele: "Niliposimamia Ukhalifa, kuna kundi lililotengua (kiapo chake) na kundi jingine lilitoka, na wengine wakafanya ujeuri, kama kwamba wao hawakuyasikia maneno ya Mwenyezi Mungu aliposema, Hayo ni makazi ya akhera tunawapa wale wasiotaka ukubwa katika nchi wala uovu, na marejeo (mema) ni kwa ajili ya wamchao Mwenyezi Mungu. Bila shaka Wallahi Wallahi, waliyasikia maneno hayo na wakayafahamu, lakini dunia imewapendeza machoni mwao na mapambo yake yamewafurahisha."[1]

Na amesema tena (Imam Ali a.s.) kuwahusu hao Masahaba: "Wamemfanya shetani kuwa ndiyo msimamizi wa mambo yao, naye amewafanya wao kuwa ni washirika (wake) basi ametaga (mayai) na kuyaangua ndani ya nyoyo zao na anatambaa ndani ya akili zao, basi (shetani) anaona kwa kutumia macho yao na anazungumza kwa kupitia ndimi zao, akawapoteza na kuwapambia maovu yakawa ndiyo matendo ya yeyote aliyeshirikishwa na shetani ndani ya utawala wake na akazungumza batili kwa ulimi wake." [2].

 

 

 

 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 next